25.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Rishard: Hatujatoka kwenye reli VPL

Theresia Gasper-Dar es SalaaM

KOCHA Mkuu wa Tanzania Prisons, Mohammed Rishard ‘Adolf’, amesema atahakikisha wanakuwa makini katika mechi zao za Ligi Kuu Tanzania Bara, ili wapate pointi tatu muhimu na kujiweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo.

Prisons ilipoteza mchezo wake uliopita wa Ligi Kuu ikiwa nyumbani dimba la Sokoine jijini Mbeya, baada ya kuchapwa mabao 3-2 na Namungo.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Adolf alisema licha ya kupata matokeo yasiyoridhisha wataendelea kuwa makini ili wawe na matokeo kama ilivyokuwa awali.

“Hivi karibuni tumekuwa na matokeo ambayo siyo mazuri lakini naamini tutaendelea kufanya vizuri katika mechi zetu zinazotukabili mbele yetu ili tuvune pointi tatu muhimu,” alisema.

Alisema kwa sasa ameendelea kuyafanyia kazi baadhi ya mapungufu yaliyojitokeza katika mechi za nyuma ili yasijirudie kwa mara nyingine.

Adolf aliwataka mashabiki wa timu hiyo waendelee kuwapa sapoti ili wachezaji wawe na morali na kuamka tena katika michezo yao.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,530FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles