RIPOTI: UCHUMI WA TANZANIA NGANGARI

0
589

Na Mwandishi Wetu,

TANZANIA yaendelea kufanya vizuri katika uchumi wake kwa kuongeza mauzo ya nje na kupunguza matumizi.

Kwa mujibu wa Ripoti ya Benki Kuu (BOT) iliyotolewa wiki iliyopita ya Mei mwaka huu, inaonyesha  kuwa mauzo ya bidhaa nje yalifikia Dola za Marekani milioni 8,753.3 kwa mwaka ulioishia April 2017, ulikilinganisha na Dola milioni 9,333.2 kwa Aprili mwaka 2016.

Ripoti hiyo imebainisha kuwa mauzo ya bidhaa asilia  kama pamba, kahawa, chai, tumbaku na korosho yaliongezeka hadi Dola milion 863.6 kutoka Dola milioni 739.7, kwani zao la korosho ndilo lililotia fora kwa kufikia dola milioni 341.1 ikilinganishwa na dola milioni 185.9 mwaka ulioishia Aprili 2016, ikiwa ni ongezeko la zaidi ya dola milioni 120.

Ongezeko hilo la mauzo ya nje ya korosho ilitokea katika uwingi wa zao na kiwango cha bei, ikitofautisha mauzo ya nje ya karafuu, katani, chai na tumbaku ambayo yalipungua kwa vigezo vyote viwili.

Bidhaa zisizo asilia thamani ya mauzo ya nje yalifikia jumla ya dola milioni 3,814.4 kutoka dola milioni 4,505.8 kwa mwaka ulioishia Aprili mwaka jana.

Mauzo ya madini ya dhahabu nje yaliongezeka kwa asilimia 26.8 kwa jumla ya dola milioni 1.515 kutoka dola milioni 1.194.6. Mauzo ya makinikia hayakuainishwa ingawa kuna kontena 277 zilizokwama bandarini.

Hata hivyo, bei ya dhahabu katika soko la dunia ilikuwa  wastani  wa dola milioni 1,260.6 kwa wakia ikilinganishwa  na mwaka ulioishia Aprili mwaka 2016.

Kwa upande mwingine, mauzo ya nje ya bidhaa za viwandani kama mafuta ya kula, nguo na bidhaa za vyuma yalipungua kutokana na kuongezeka kwa ushindani katika masoko la kikanda ambapo bidhaa nyingi za viwandani kuuzwa nje na zinafanana.

Kwa upande wa sekta ya utalii katika (Tourism Exports Travel), mauzo yaliongezeka kidogo kwa kiasi cha dola milioni 2,131 kutoka dola milioni 2,105 kufuatia ongezeko la idadi ya watalii waliofika nchini.

Kwa upande wa ripoti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), inaonyesha kuwa kwa mwaka 2016, Pato la Taifa (GDP) lilikua kwa wastani wa asilimia 7 sawa na 2015 na IMF inadai hali hiyo itaendelea kwa mwaka wote.

Ukuaji wa GDP  unatokana na kuongezeka kwa uzalishaji umeme hasa kutumia gesi asilia ambapo kulichangia kuongezeka kwa uzalishaji wa viwandani, kuboresha huduma za usafiri katika Jiji la Dar es Salaam na kuongezeka kwa uandikishaji wa watoto katika elimu ya msingi kuanzia Januari 2016, baada ya kutangazwa kutoa elimu bila malipo.

Shughuli za kiuchumi mwaka jana ambazo zilionyesha kiwango cha ukuaji ni pamoja na sekta ya ujenzi kwa asilimia (13), mawasiliano ( 13), usafirishaji wa mizigo na kuhifadhi (11.8) na madini na uchimbaji (11.5).

Shughuli za kilimo nchini zilionyesha kuongezeka kwa asilimia 2.1 mwaka jana ikilinganishwa na asilimia 2.3 mwaka 2015, kutokana na ukosefu wa mvua ya kutosha katika msimu 2015/16 wa kilimo.

Kiwango cha ukuaji wa pato la Taifa kwa wastani asilimia 7 katika kipindi cha miaka mitano na kuifanya Tanzania kuwa miongoni  mwa nchi 20 zinazokua kwa kasi katika uchumi duniani.

Athari ndogo ya kukua uchumi

Watanzania wengi huwa wanakosa kuelewa ukuaji wa uchumi wa Tanzania na kuhoji mbona neema hiyo haiko wazi kwa kila mwananchi.

Ukweli ni kuwa kama taarifa mbalimbali zilivyoanishwa hapo juu, ukuaji mkubwa hauko kwenye sekta zile za watu wengi kama kilimo na hivyo kukosa kuwafikia wengi.

Kama kilimo shughuli zake zingekuwa kwa asilimia kubwa, watu wengi wangepata matokeo chanya na hivyo kufanya wataalamu wa uchumi waishauri Serikali kuwekeza zaidi kwenye kilimo kwani matokeo yake yanawafikia wengi. Na kwenye kilimo hicho si kung’anga’ania mazao ya asili bali yale yanayohitajika kwenye soko kama mbogamboga na matunda chini ya TAHA yameweza kuingiza zaidi ya dola milioni 645 kwa mwaka jana pekee.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here