22.4 C
Dar es Salaam
Sunday, May 12, 2024

Contact us: [email protected]

RIO FERDINAND UMRI UTAMUUMBUA KWENYE NGUMI?

NA BADI MCHOMOLO


WATAALAMU wa mambo wanadai kuwa ili ufanikiwa hasa kwenye michezo unatakiwa kuanza kujifunza tangu ukiwa na umri mdogo chini ya miaka 20.

Watu wengi chini ya umri huo akili yao inakuwa nyepesi kuelewa jambo na kulishika, pia wanakuwa hawana mambo mengi sana ya kufikiria juu ya maisha yao na vitu vingine.

Madhara ya kujifunza vitu ukiwa na umri mkubwa ni kwamba unaweza kuchelewa kujua, ukawa na uelewa mdogo, kuwa msahaulifu na mambo mengine, lakini unaweza kufanikiwa ila sio kwa asilimia kubwa sana.

Aliyekuwa beki wa kati wa klabu ya Manchester United na timu ya Taifa ya England, Rio Ferdinand, alitangaza kustaafu soka mwaka 2015 baada ya kuitumikia klabu ya QPR kwa msimu mmoja.

Wachezaji wengi wa soka wanaonekana wakikimbilia kwenye uchambuzi wa michezo au uongozi wa timu kama kuwa makocha.

Lakini hali imekuwa tofauti kwa beki hiyo wa zamani ambaye alikuwa na jina kubwa sana ndani ya Old Trafford chini ya kocha wao Sir Alex Ferguson, kwa upande wake yeye ameamua kujitupia kwenye ngumi.

Ferdinand kwa sasa ana umri wa miaka 38, hivyo aliamini kuwa umri wake unamtupa mkono na atakuwa na wakati mgumu wa kukimbizana na wachezaji wenye umri chini ya miaka 30, kwa kuwa wanakuwa na pumzi za kutosha.

Yalikuwa ni maamuzi sahihi kwa mchezaji huyo na wengi walimuunga mkono hata kama kwa shingo upande kwa kuwa bado walikuwa wanahitaji huduma yake uwanjani.

Hajakosea kustaafu soka kutokana na sababu ya umri, lakini anaweza kuwa anakosea kukimbilia kwenye ngumi kwa umri alionao.

Ngumi ni miongoni mwa michezo ambayo inahitaji bondia kuwa na pumzi, hivyo kama Ferdinand aliamua kuachana na soka kwa kuhofia pumzi hata kwenye ngumi kunahitaji pumzi za kutosha.

Hata hivyo suala kubwa sio tu pumzi, lakini umri alioanza kujifunza ngumi ni mkubwa sana hivyo atakuwa na wakati mgumu wa kupambana na wale ambao walianza mchezo huo wakiwa na umri chini ya miaka 20.

Kama ameamua kukimbilia kwenye ngumi ikiwa ni sehemu ya starehe au ni mchezo ambao ulikuwa kwenye kichwa chake kuwa lazima aje kuujua, sio tatizo kubwa, ila kama anataka kuingia kwenye ushindani atakuwa na wakati mgumu.

Wenzake wenye umri huo tayari wana mataji mbalimbali ya ngumi na wana uzoefu wa muda mrefu, hivyo itakuwa ngumu kwa yeye kutwaa ubingwa kwa urahisi.

Hata hivyo itakuwa ngumu kupata jina zaidi kwenye mchezo huo, ila jina lake litaendelea kuwepo kutokana na yale aliyoyafanya katika maisha yake ya soka.

Mwezi mmoja uliopita bingwa wa mchezo wa ngumi mchanganyiko kutoka nchini Iralend Conor McGregor, alishuka ulingoni kwa mara ya kwanza kupigana na bingwa wa ngumi za kawaida Floyd Mayweather, lakini McGregor alichezea kichapo kutokana na kukosa uzoefu wa aina ya ngumi hizo.

Inawezekana kama angekuwa amewahi kucheza mara kwa mara angefanikiwa, kwa kuwa alikuja kupigwa kwenye raundi ya 10 kati ya 12.

Wapo wanasoka mbalimbali ambao walitangaza kustaafu soka na baadae wakaamua kukimbilia kwenye ngumi, lakini mafanikio yao hayakuwa makubwa sana.

Curtis Woodhouse, alikuwa nyota wa soka wa klabu ya Hull City, uwezo wake ulikuwa mkubwa kwenye safu ya kiungo na alipata mafanikio makubwa, lakini baada ya kustaafu soka aliingia kwenye ngumi uzani wa lightwelterweight na baadae kurudi kwenye soka kama kocha kutokana na kushindwa kufanya vizuri kwenye ngumi.

Andrew Flintoff alikuwa nyota wa mchezo wa Kriketi, baada ya kustaafu aliingia kwenye ngumi na kufanikiwa kumpiga mpinzani wake Richard Dawson katika raundi nne kwenye uzani wa heavyweight mwaka 2012.

Mabondia mbalimbali wanaonekana kusapoti maamuzi ya Ferdinand kuingia kwenye ngumi, labda inawezekana wanamkaribisha ili iwe sehemu ya wao kujichukulia pointi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles