RIHANNA HATAKIWI SENEGAL

0
1007

DAKAR, SENEGAL


NYOTA wa muziki nchini Marekani, Robyn Fenty ‘Rihanna’, anatarajiwa kuhudhuria mkutano mkubwa nchini Senegal mwezi huu, lakini vikundi vya dini nchini humo vimekataa kumpokea.

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Jeune Afrique, baadhi ya madhehebu ya dini nchini humo yanaamini kuwa msanii huyo anajihusisha na mambo ya kishetani kama vile Freemason.

“Tumeukataa ufreemason na mapenzi ya jinsia moja hapa nchini, kuna taarifa kwamba msanii huyo ni mjumbe wa chimbuko la Illuminati linaloaminika kuwa ni kundi maalumu la watu ambao hudhibiti masuala na uongozi wa dunia na kutaka utawale uongozi wao,” vilisema vikundi 30 vya kidini.

Rihanna atatembelea nchi hiyo ya Afrika Magharibi akiwa katika wadhifa wake wa balozi wa Shirika la Elimu ‘Global Partnership Foundation’.

Shirika hilo lina lengo la kuchangisha fedha za kuwafundishia mamilioni ya watoto na vijana katika nchi zinazoendelea.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here