23.8 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

BABA ADAI RANGI IMEMSAIDIA BEYONCE KUWA MAARUFU

NEW YORK, MAREKANI


BABA wa nyota wa muziki nchini Marekani, Beyonce, Mathew Knowles, amezungumzia ubaguzi wa rangi nchini humo na kudai watoto wake, Beyonce na Solange wasingeweza kuwa maarufu kama wangekuwa na rangi nyeusi.

Mzee huyo amesema wasanii wote weusi wa kike wenye majina makubwa nchini humo rangi zao zinang’aa kutokana na kuchanganya wazazi na bila hivyo wasingeweza kutamba.

“Ni wazi kwamba wasanii wa kike ambao ni weusi na wanafanya vizuri kwenye radio ni pamoja na Mariah Carey, Rihanna, Nicki Minaj na watoto wangu Beyonce na Solange.

“Mara ya kwanza nakutana na mama wa Beyonce nilidhani kuwa ni ngozi nyeupe, lakini baada ya kukaa naye kwa muda nikagundua kuwa sio, ila baada ya kuchanganya rangi yangu na yake tukafanikiwa kupata watoto ambao wanang’aa, lakini bila rangi hiyo wasingeweza kuwa na majina makubwa,” alisema Mzee huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles