20.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, July 5, 2022

Repoa: Ipo haja kuchambua viashiria vingi vya uchumi

Na CHRISTINA GAULUHANGA -DAR ES SALAAM

TAASISI ya Utafiti ya Kuondoa Umasikini (Repoa) imesema ipo haja kwa wachambuzi kuangalia kwa makini viashiria zaidi ya kimoja vinavyochochea ukuaji wa uchumi.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Repoa, Dk. Donald Mmari, alisema ni vyema kuangalia uchumi wa ndani kwa kuanzia ngazi ya chini.

Alisema kila mmoja akiwa mshiriki katika ukuaji uchumi kwa kuibua fursa na kuzitambua, kila eneo lina uwezo wa kuchochea uchumi kukua.

 “Ni bora kuangalia namna bora ya kuangalia fursa katika ukuaji uchumi na sisi kama Repoa tumejipanga kufanya tafiti za kiuchumi zenye matokeo mazuri ndani ya jamii,” alisema Mmari.

Alisema atahakikisha matokeo ya tafiti zao zinawafikia wananchi wote ili kuondoa changamoto zilizopo.

 “Mfumo wa Serikali kwa upande wa halmashauri si rahisi kufanya katika shughuli za kiuchumi kutambua fursa, kujenga uwezo wenye tija zaidi,” alisema Mmari.

Naye Mkurugenzi wa Tafiti za Kimkakati, Dk. Jamal Msami, alisema unapozungumzia maendeleo ni vyema kuangalia mifumo inayotumika katika halmashauri zote ili kubaini jambo hilo.

Alisema ipo haja ya upatikanaji na uendelezaji fursa ili zilete matokeo ndani ya jamii.

 “Hapa nchini kuna halmashauri 185 na kwa Tanzania Bara na Visiwani kuna mikoa 31 hivyo ni vyema kufungua fursa zilizopo ili kuondoa mkwamo na kufikia maendeleo,” alisema.

Akizungumzia mkutano wa 24 wa ripoti ya utafiti wa mwaka unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao, Mkuu wa Utafiti wa Repoa, Dk. Brandina Kilama, alisema mkutano huo utashirikisha wachambuzi makini wa masuala ya uchumi.

Alisema Repoa imelenga kuangalia kila nafasi ina wajibu gani katika kukuza uchumi wa nchi kwa maendeleo ya uchumi wa ndani.

Pia alisema ni vyema kukawa na ushirikishwaji na upatikanaji wa fursa kuanzia ngazi ya chini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
195,686FollowersFollow
545,000SubscribersSubscribe

Latest Articles