24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Rekodi zaibeba Stars ikikabili Burundi leo

NA SOTHENES NYONI-DAR ES SALAAM

TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo itashuka dimbani kuumana na Burundi, katika pambano la kirafiki la kimataifa la kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa(Fifa), litakalochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Mgeni rasmi katika mchezo huo ambao unatarajia kupigwa kuanzia saa 10 kamili jioni atakuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Stars itajitupa uwanjani ikijivunia  rekodi yake nzuri dhidi ya Burundi, zilipokutana katika mashindano mbalimbali na michezo ya kirafiki.

Rekodi zinaonyesha, tangu mwaka 1971, Stars na Burundi ambayo kwa jina la utani inafahamika Intamba Murugamba, zimekutana mara 19.

Katika kukutana huko, Stars imeshinda michezo 12, imechapwa mara tano na mara tatu zikitoka sare.

Michezo hiyo inahusisha ile ya kirafiki, Kombe la Chalenji ya Baraza la Vyama vya Soka kwa Nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, kufuzu fainali za Kombe la Afrika na Kombe la Dunia.

Pia katika michezo 12 ambayo zimekutana katika ardhi ya Tanzania, Stars imeshinda tisa, Burundi ikaibuka mbabe mara tatu na mara moja mchezo ukimalizika kwa sare.

Stars na Burundi zilikutana mara ya mwisho Septemba 8, mwaka jana, katika mchezo wa kusaka tiketi ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia, zitakazofanyika mwaka 2022 nchini Qatar, uliopigwa Uwanja wa Taifa(sasa Mkapa).

Mchezo huo ulimalizika kwa Stars kuibuka na ushindi wa penalti 3-0.

Huo ulikuwa mchezo wa marudiano, baada ya ule wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Intwari nchini Burundi kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Ushindi ni muhimu kwa Stars katika mchezo huo, ili kuongeza morali ya kikosi inaposubiri kuumana na Tunisia, katika mchezo wa kusaka tiketi ya kufuzu fainali za mataifa ya Afrika, utakaopigwa Novemba 13, mwaka huu.

Katika mchezo huo, Stars itaanzia ugenini kabla ya mchezo wa marudiano kupigwa  nyumbani Tanzania.

Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo, mlinda mlango namba moja wa Stars, Aishi Manula aliwaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi kuwashangilia ili kuwaongezea nguvu ya kupambana kusaka matokeo mazuri kwenye mchezo huo.

Manula alisema wanafahamu mchezo wao na Burundi utakuwa mgumu lakini kwa sababu wanakitu wanahitaji watapigana kwa jasho na damu.

“Tutapambana kwa jasho na damu mbele ya Burundi, huu ni mchezo muhimu sana kwa sababu ndio itakayotupa uelekeo katika mashindano ya yanayokuja.

“Tunawaomba mashabiki waje kutupa sapoti,huku wakiwa na imani na wachezaji kuwa tunaweza kuwapa ushindi,”alisema Manula.

Kwa upande wake, Kocha Msaidizi wa Stars, Selemana Matola, alisema ana matumaini makubwa ya kupata ushindi katika mchezo huo kutokana na maandalizi waliyoyafanya.

“Wachezaji wamekuja kutoka katika klabu zao wakiwa na viwango vizuri , hii imetusaidia kutengeneza muunganiko kwa haraka ambao utatupa matokeo ya ushindi Jumapili (leo).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles