23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

RC Mwanza awafunda viongozi wa dini

Na Sheila Katikula, Mwanza

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Robert Gabriel amewataka waumini na viongozi wa dini  kumtumikia Mungu kwa nyakati zote kwa kutenda mambo mema na siyo kufuata mafundisho ya walimwengu yanayolenga kupotosha imani na amani iliyopo.

Viongozi mbalimbali wa dini ambao ni wahitimu ya Masomo ya Biblia katika chuo cha Grace International Bible University wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel. PICHA na Sheila Katikula

Gabriel amesema hayo Jumanne Julai 20, 2021 kwenye mahafali ya kwanza kwa kanda ya Mwanza  ya Chuo cha Grace International Bible University na kusisitiza kwa muda wote kwenye maisha ya kila siku kila mmoja anao wajibu wa kujitolea kufanya kazi za mwenyezi Mungu bila kujali nafasi aliyonayo.

Aidha mkuu huyo wa mkoa amewaomba waumini na viongozi wa dini kuwa wavumilivu na kujiamini katika kumuabudu mungu kwa kujisimamia bila kuogopa changamoto yoyote na kujenga utamaduni wa kujitolea kwa ajili ya maendeleo ya kanisa na taifa kwa ujumla.

Katika hatua nyingine, kutokana na Chuo hicho kukosa eneo la kujenga ofisi za ziada na madarasa, Gabriel amemuagiza Katibu Tawala wa mkoa kuhakikisha anatafuta eneo la hekai 20 lililopo karibu na ziwa ili waweze  kujenga  na kuepuka kusomea kwenye majengo ya  kanisa la EAGT Bugando kama ilivyo hivi sasa.

Mkuu wa Chuo cha Grace International Bible University, Dk Joel Nteminyanda alisema elimu ya dini inasaidia kupata ufahamu mzuri hekima na maarifa ya kujua mema na mabaya ambayo yanaisaidia jamii kutoenekeza matendo yasiyompendeza Mwenyezi Mungu, hivyo kila mtu anawajibu wa kutambua umuhimu wa kupata elimu ya dini.

Naye Mwenyekiti wa Chuo hicho, Askofu Boaz Kilayi  alisema amejifunza mambo mbalimbali kutoka chuoni hapo na imemusaidia kupanua ufahamu  na uelewa wa huduma zaidi tofauti na hapo awali, kwa hiyo ni vyema vijana wahamasike kupata elimu ya dini kwani elimu ndio msingi wa maarifa na kumcha Mungu. 

Awali akisoma risala ya mahafari hayo, mhitimu wa masomo ya biblia, Leah Mwafilombe alisema jumla ya wahitimu 31 wamehitimu ngazi mbalimbali ambapo astashahada kuna wahitimu wawili, shahada ya kwanza wahitimu 14  na shahada ya pili ni wahitimu 15.

Kwa upande wake mhitimu wa Chuo hicho Clement  Pancrasalisema kutokana na umuhimu wa elimu ni vema wazazi na walezi kujiendeleza wao na familia zao ili waweze kupata maarifa na maadili yanayofundishwa kutoka kwenye chuo hicho.   

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles