23.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 3, 2023

Contact us: [email protected]

RC Kunenge asikitishwa na ujenzi Barabara ya Goba

Na Brighter Masaki, Dar es Salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge, ametoa maagizo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kuhakikisha anasimamia miradi ya barabara ili ikamilike kwa muda waliokubaliana.

Akizungumza mapema leo Jumatatu Machi 1, kwenye ziara ya kukagua miundombinu ya barabara za Wilaya hiyo, Kunenge ameoneshwa kusikitishwa kwake na maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Goba- Makongo yenye urefu wa kilometa 8.5 inayojengwa kwa awamu.

Mpaka sasa Mkandarasi wa mradi huo, Jessie Company Ltd, amejenga kilometa moja tu kati ya kilometa 4.58 huku tatu zikisalia kutokana na changamoto za ulipaji fidia kwa nyumba zinazotakiwa kbomolewa.

Kunenge amesema mradi huo unafadhiliwa na Serikali ni wajibu kwa kila kiongozi kutimiza majukumu yake kuhakikisha wanainchi wanapata huduma.

“Mkuu wa Wilaya nakuomba simamia mradi huu kwa kushirikiana na Wakala wa Barabara (Tanroads) ukamilike kwa wakati kama kunachangamoto za ulipaji wa fidia kama anavyosema mkandarasi basi malizeni haraka, wananchi wanahitaji huduma hawajui hizi changamoto nyingine,” amesema Kunenge.

Aidha gharama za mradi huo ambao ulianza Januari 2019 ni Sh bilioni 8 na muda wa mkataba ni miezi 12 lakini wameongezewa miezi 11.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles