28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

RC Homera awaalika Watanzania Hifadhi ya Katavi

Mwandishi Wetu, Katavi

Watanzania wametakiwa  kujijengea utamaduni wa kufanya utalii wa ndani kwa kutembelea hifadhi mbalimbali za taifa zilizopo nchini hususani Hifadhi ya Katavi.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Juma Homera ametoa wito huo jana akihamasisha Watanzania kutembelea vivutio  vilivyopo katika mkoa huo ikiwamo Hifadhi ya Taifa ya Katavi na fukwe za Ziwa Tanganyika na kuwekeza kibiashara.

“Nitoe wito kwa Watanzania na watu mbalimbali kuja kutembelea vivutio vilivyopo katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi ili kujionea aina mbalimbali za wanyama wanaopatikana katika mbuga hii  wakiwamo Twiga weupe ambao hupatikana katika hifadhi hii pekee.

“Pia licha ya vivutio vilivyopo vya mbuga pia amewataka wadau kuja kuwekeza katika biashara ya utalii kwa kujenga hoteli, Campsite na magari ya kusafirishia watalii,” amesema.

Amesema Mkoa wa Katavi una fursa nyingi ikiwamo uchimbaji wa madini hivyo kuwakaribisha wawekezaji wa madini kufika kuwekeza katika Mkoa wa Katavi ambao una mandhari nzuri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles