28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

RC Chalamila aonya wazazi wanaoozesha watoto nakusingizia wamepotea

Na Renatha Kipaka, Bukoba

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Erasto Sima kushirikiana na Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani humo, Wiliam Mwampaghale kufanya ufuatuliaji kwa wazazi wanaokiuka haki na sheria ya kusomesha watoto.

Chalamila ametoa agizo hilo Januari 30, 2023 wakati akiwaapisha Wakuu wapya wa Wilaya za Muleba, Karagwe na Biharamlo walioteuliwa hivi karibuni na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ambo wanaelekea.

“Inauma sana ninapoona baadhi ya wazazi ndani ya mkoa huu eti hawapendi watoto wao wasome na badala yake wanakwenda kuwaozesha, hiyo haikubariki,”amesema Chalamila.

Amesema kumekuwapo na tabia za wazazi kutafuta RB katika kituo cha polisi kwa kusingizia kwamba wamepotelewa na watoto wao wamepotea jambo ambalo siyo kweli.

“Kuna vijitabia vimezuka sasa wazazi wanakwenda kuchukua RB kituoni eti wamepotelewa na watoto kumbe wamewaozesha tayari ili asisumbuliwe, akija mtu wa aina hiyo kamata alafu mtafute na Mwenyekiti wake ili tukomeshe vitendo hivi vinavyo wafanya vizazi vya kesho kutokufikia malengo,” amesema Chalamila.

Aidha, katika Kijiji cha Karonge kata Ibwera, wazazi waliozesha mtoto, mahari walipokea na wakafunga ndoa lakini wazazi wake katika maelezo wanadai binti yao anaishi mkoani Mwanza kitu ambacho sio kweli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles