23.3 C
Dar es Salaam
Sunday, June 16, 2024

Contact us: [email protected]

Chongolo aitaka Tanroad kumbana Mkandarasi Kilombero

Na Ashura Kazinja, Kilombero

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo ameisisitiza Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kumsimamia kikamilifu Mkandarasi anayejenga kwa kiwango cha lami barabara ya Kidatu – Ifakara yenye urefu wa kilomita 66.9 ili aweze kukamilisha kazi kwa muda sahihi uliopangwa na Serikali.

Akizungumza na mapema leo Januari 31, 2023 baada ya kuwasili wilayani Kilombero akitokea wilayani Kilosa, Chongolo amesema haiwezekani ujenzi huo uchelewe wakati fedha za utekelezaji wake tayari zilishatengwa huku akiwaonya wasimamizi watakao kaidi maelekezo hayo ya chama.

Hata hivyo, amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Fatma Mwasa kukaa na viongozi wa vyama vya wakulima (AMCOS) ili kuona namna ya kuwapa elimu bora ya kuzalisha miwa yenye kiwango kikubwa cha Sukari ili kuondoa changamoto ya ukosefu wa utamu kwenye miwa.

Naye Mbunge wa jimbo la Kilombero, Aboubakar Assenga ameiomba TANROADS kuharakisha ujenzi wa barabara hiyo ili iweze kuwasaidia wakulima kurahisisha usafirishaji wa bidhaa zao kwenye masoko mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.

Alisema wilaya hiyo inayojishugulisha na kilimo ikiwa na uwekezaji wa viwanda vya sukari Kilombero na Ilovo inakabiliwa na changamoto za utamu kwenye sukari, barabara na soko la bidhaa zao ambalo aliahidi kulipatia ufumbuzi mapema.

Akizungumza kwenye kikao hicho mbunge wa Mikumi, Denis Londo ameishukuru Serikali kwa kuona umuhimu wa kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami ili kurahisisha mawasiliano kati ya Wilaya ya Kilombero na Kilosa kupitia daraja la kidatu ambalo nalo limefanyiwa marekebisho maboresho.

Upande wake Meneja wa TANRODS mkoa wa Morogoro, Mhandisi Alinanuswe Kyamba amesema ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami ulioanza kutekelezwa tangu mwaka 2017 na ulitakiwa kukamilika mwaka 2020 kwa gharama ya Sh bilioni 105.035 za Tanzania ambapo inatarajiwa kukamilika Oktoba, 2023.

Amesema utekekezaji wa mradi huo katika kipindi cha Januari hadi Desemba mwaka 2022 umezalisha ajira 903 ambapo kati ya hizo ni wanawake 191 na wanaume 712.

Aidha, alisema katika kutekeleza ujenzi wa barabara hiyo serikali ililipa fidia kiasi cha Sh bilioni 2.6 kwa waathirika mbalimbali mwaka 2018 na mwaka 2019.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles