Rayuu wa mitandaoni na nyumbani ni tofauti!

0
1212

8977c613656d96073d7015b7676fe2b1NA CHRISTOPHER MSEKENA

MAKUBWA! Mrembo anayetikisa kiwanda cha filamu nchini, Rahma Rayuu ‘Rayuu’ amesema maisha yake halisi na maisha anayoonyesha kwenye mitandao ya kijamii ni tofauti hivyo watu wanaodhani ndivyo alivyo wanakosea.

Akichonga na Swaggaz, Rayuu alisema kuwa amezoea kuweka mitandaoni picha zinazoonyesha mwili wake lakini kiuhalisia ni mtu mwenye maadili ambaye akiwa nyumbani huvalia hadi ushungi kujisitiri.

“Kwetu ni familia ya dini na nimekuwa kwenye mazingira hayo, kule kwenye mitandao ni mazoea tu yananifanya niweke picha kama zile… mimi ni binti mwenye maadili mema,” alisema Rayuu.

Hivi mmemuelewa lakini? Dizaini kama haeleweki vile.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here