23.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 10, 2022

RAIS WA ALGERIA AGEUKWA NA CHAMA CHAKE

Na Mwandishi Wetu

Chama cha Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika kimekataa mpango wa Rais huyo wa kutaka kuanzisha baraza la kitaifa lenye lengo la kuzima maandamano makubwa ambayo yamekuwa yanafanyika kupinga uongozi wake.

Msemaji wa chama hicho, FLN alieleza kupitia kituo cha televisheni kwamba baraza hilo halina maana tena kwa sababu litawahusisha wajumbe ambao hawakuchaguliwa, jambo ambalo linapingwa na waandamanaji.

Msemaji huyo, Hocine Khaldoun amesema suluhisho la mgogoro wa kisiasa nchini Algeria litapatikana kwa kuchaguliwa Rais mwenye uwezo wa kuzungumza na wananchi.

Kauli hiyo ni pigo jingine kwa Bouteflika mwenye umri wa miaka 82, ambaye ameonekana hadharani kwa nadra tangu alipopata ugonjwa wa kiharusi mwaka 2013.

Bouteflika alifuta uchaguzi uliokuwa ufanyike Aprili 18 na badala yake kalipendekeza kuundwa kwa kamati ya kitaifa yenye wawakilishi kutoka nyanja zote za jamii ili kutayarisha uchaguzi mpya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,395FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles