24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Samia aweka Bilioni 6.2 ujenzi wa mabwawa nchini

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Serikali inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuboresha kila sekta nchini ambapo imetenga Sh bilioni 6.2kwa ajili ya kujenga mabwawa ya kunyweshea mifugo kote nchini.

Hayo yameelezwa Februari 17, 2023 na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega (Mb) alipokuwa akizungumza kwenye ziara ya kikazi kukagua maendeleo ya ujenzi wa bwawa la maji la Kwekinkwembe lililopo katika Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga.

Naibu Waziri Ulega amesema Rais Dk. Samia katika bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2022/23 ameridhia kuipatia wizara Sh bilioni 6.2 kwa ajili ya ujenzi wa mabwawa hayo.

Alifafanua kuwa kila sekta nchini imeguswa ikiwemo ya mifugo na kwamba hakuna iliyeachwa nyuma hivyo wafugaji watanufaika kwa kupata maji ya uhakika mara baada ya mradi wa ujenzi wa mabwawa ya kunyweshea mifugo maji kukamilika.

“Rais Dk. Samia hakuna aliyemuacha pembeni ndiyo maana amegusa wakulima mbegu za ruzuku, amegusa wafugaji mabwawa na majosho, hivyo hakuna aliyeachwa nyuma,” amesema Ulega.

Aidha, amemtaka mkandarasi anayefanya shughuli za ujenzi wa bwawa hilo kuhakikisha anatoa taarifa ya kila hatua ya ujenzi na kuacha nakala wilayani hadi ngazi ya kijiji kunapojengwa bwawa hilo ili taarifa ziwe wazi na kumtaka kukamilisha ujenzi kwa wakati.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Abel Busalama amewataka wananchi wa Kijiji cha Kwekinkwembe kuhakikisha bwawa hilo linalojengwa kwa thamani ya Sh bilioni 504 mara litakapokamilika walisimamie vyema ili liwe na tija kwao.

Amesema uongozi wa kijiji utapaswa kuweka utaratibu mzuri wa namna ya kulitumia na kuliongezea thamani kwa kuyafanyia pia maji hayo shughuli mbalimbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles