31.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Raia wa Msumbiji wachagua hatma yao

Maputo, Msumbiji

IKIWA ni miezi michache tangu Agosti, chama  tawala cha Msumbiji na upinzani waliposaini mkataba kufuatia machafuko ya miaka 15, jana raia wa nchi hiyo walipiga kura kuchagua viongozi watakaoongoza taifa hilo kwa miaka mitano ijayo.

 Rais Felipe Nyusi anatarajiwa kushinda awamu ya pili ya uongozi.

Mustakabali wa kisiasa wa Msumbiji utajulikana baada ya wapigakura takriban milioni 13 kupiga kura kuchagua wawakilishi wao kuanzia rais, wabunge na wawakilishi wa mikoa.

Uchaguzi huo unaonekana kama mtihani kati ya chama tawala nchini humo na upande wa upinzani baada ya kutia saini mkataba wa amani Agosti kufuatia machafuko ya miaka 15 yaliyoizonga nchi hiyo na kusababisha vifo vya takriban watu milioni moja.

Rais Nyusi anatarajiwa kupata changamoto kutoka kwa kiongozi wa upinzani Ossufo Momade wa chama cha Renamo.

Chama cha Momade kinaonekana kupata umaarufu katika siku za hivi karibuni na anatumaini kuwa umaarufu huo huenda ukamsaidia.

Mgombea mwengine wa urais ni Meya wa Mji wa Beira, Daviz Simango wa chama cha upinzani cha MDM.

Rais Nyusi ametaka raia wa nchi hiyo kuwa watulivu na kuwatolea wito wa kudumisha amani, ikiwa ni wiki moja tu baada ya Idara ya Polisi kuthibitisha kuwa baadhi ya polisi wanashukiwa kuhusika na mauaji ya mwangalizi maarufu wa uchaguzi, Anastacio Matavel.

“Nawatakia kila la heri raia wa Msumbji, natumaini uchaguzi huu utakwenda vizuri. Na mgombea bora ashinde, mgombea mwenye mawazo bora, ilani bora na mpango bora kwa watu wa Msumbiji. Asanteni,” alisema Rais Nyusi.

Mauaji ya Matavel yamelaaniwa vikali na waangalizi wa kimataifa wa uchaguzi na pia yamepandisha joto la kisiasa nchini humo.

Hali hiyo huenda ikawatia hofu baadhi ya wapigakura ambao huenda wakakosa kujitokeza kutekeleza wajibu muhimu wa kushiriki uchaguzi.

Tume ya Uchaguzi imevifunga takriban vituo 10 vya kupigia kura katika Wilaya ya Kaskazini ya Cabo Delgado kutokana na ukosefu wa usalama.

Vituo vya kupigia kura vitafungwa saa kumi na moja jioni saa za Msumbiji wakati ambapo uhesabuji kura unatarajiwa kuanza huku matokeo ya awali yakitarajiwa kutolewa Jumatano.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles