EU: Mkataba wa Brexit unaweza kufikiwa wiki hii

0
432
Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya kwenye mazungumzo ya Brexit, Michael Barnier

Brussels, Ubelgiji

UMOJA wa Ulaya (EU) umesema mkataba wa Brexit unaweza kufikiwa wiki hii, lakini mapendekezo ya Serikali ya Uingereza hayajitoshelezi kuwezesha kupatikana kwa makubaliano.

Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya kwenye mazungumzo ya Brexit, Michael Barnier, alisema kuelekea mkutano wa mawaziri wa mambo ya kigeni wa umoja huo, changamoto kubwa ni kubadili mapendekezo ya Uingereza kuhusu suala tata la mpaka wa Ireland mbili kuwa mkataba.

Kuhusu matarajio ya mkutano huo, Barnier alisema hata kama mkataba utakuwa mgumu, unawezekana kufikiwa wiki hii.

Viongozi wa Umoja wa Ulaya watakutana kwa mkutano wa kilele wa siku mbili mjini Brussels kuanzia Alhamisi huku suala la Brexit likitarajiwa kuwa mada kuu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here