26.2 C
Dar es Salaam
Saturday, May 4, 2024

Contact us: [email protected]

Radi yauwa watu watatu Serengeti

Na Maliama Lubasha, Serengeti

WATU watatu wakazi wa Vijiji vya Nyamburi na Tamkeri wilayani Serengeti mkoani Mara, wamefariki dunia baada ya kupigwa na radi kwa nyakati tofauti kufuatia mvua kubwa iliyonyesha katika vijiji hivyo.

Matukio hayo yamethibitishwa na wenyeviti wa kiijiji cha Nyamburi, Samson Matiko na Thomas Marwa wa kijiji cha Tamkeri na madiwani wa kata za Sedeco, Raphael Matiko na John Ghati  wa kata ya Mbalibali matukio hayo inadaiwa kuacha majonzi kwa familia hizo kupoteza nguvu kazi . 

Mwenyekiti wa kijiji cha Nyamburi, Samson Matiko amesema tukio hilo limetokea Machi 4, mwaka huu saa 12 jioni eneo la Shule ya Sekondari Nyamburi wakati baba na mtoto wakichunga ng’ombe ambapo mvua ilinyesha ikiambatana na radi na kumuua Chacha Mchongwe (30) mkazi wa kitongoji cha Saraganda katika kijiji hicho.

Matiko amesema kuwa radi hiyo ilipiga marehemu upande wa kulia kuchana sikio la kulia na kutoboa darasa na kutoka nje sekondari hiyo kwa maelezo kuwa baada ya mvua kuanza kunyesha mchongwe na kijana wake walikwenda kujikinga mvua darasani.

Alifafanua kuwa baada ya ng’ombe kwenda mbali alimtuma mtoto wake kuwarudisha ng’ombe hao huku radi zinapiga aliporejea alimkuta baba yake ameanguka chini alipojaribu kutoa msaada hakuweza kuongea hivyo aliondoka na ng’ombe kurejea nyumbani na kutoa taarifa kwa mama yake ambaye alipiga yowe na watu kuja kumpa masaada hata hivyo alikata roho akiwa njiani kupelekwa hospitali.

Mwenyekiti huyo amesema kuwa hilo ni tukio la tano watu kupigwa radi na kupoteza maisha nakwamba matukio ambayo yanahusishwa kuwepo kwa madini kutokana na imani hiyo amesema wanafunzi wa  shule hiyo wanapoona mvua inanyesha hukimbia kwa kuhofia kupigwa na radi.

Aidha, Diwani wa kata ya Sedeco, Raphael Matiko ametoa wito kwa wataalam madini kufika eneo hilo kufanya uchunguzi ili kuwatoa hofu wananchi wa kijiji hicho kama ni kweli radi zinatokea eneo hilo kwa kuwepo madini.

Katika tukio linguine limetokea katika kijiji cha Tamkeri kata ya Mbalibali siku ya Machi 22, mwaka huu saa 2 usiku ambapo radi imepiga na kuuwa vijana wawili wa familia moja wakiwa wamelala.

Mwenyekiti wa kijiji hicho, Thomas Matiko akithibitisha kutokea tukio hilo amewataja waliofariki dunia kuwa ni, Gibita Mtende(17) na Migera Mtende(15) ambao wote ni ndugu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles