Queen Darleen ammwagia sifa Harmonize

0
846

JESSCA NANGAWE

MWANADADA kutoka lebo ya WCB, Queen Darleen amefunguka kwa kummwagia sifa Rajab Abdul maarufu kwa jina la Harmonize kuwa ni msanii bora mbali ya tofauti zao.

Mrembo huyo amedai Harmonize ni mmoja kati ya wasanii wakubwa na wanaofanya vizuri japokuwa hajamfikia Diamond Platnumz.

“Siwezi kuzungumzia kuondoka kwake lakini nachoweza kusema ni msanii mkubwa, anafanya kazi nzuri na kwangu akitoka Diamond anayefuata ni yeye, unatakiwa kuweka mbali bifu na kuzungumzia ukweli wa mtu fulani lakini wanadamu wengi hatupo hivyo,” alisema Queen Darleen.

Mrembo huyo na Harmonize waliwahi kufanya kazi ya pamoja ambayo inajulikana kwa jina la ‘Mbali’ na imefanya vizuri kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here