27 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Stars yaipigia hesabu za mbali Sudan

MOHAMED KASSARA-DAR ES SALAAM

KAIMU Kocha Msaidizi wa timu ya Taifa Tanzania ‘Taifa Stars’, Juma Mgunda amesema kikosi hicho kitatumia  mchezo wao wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Rwanda, kuindalia kipigo Sudan.

 Stars inatarajia kuumana na Rwanda, katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki wa kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) utakaochezwa Oktoba 14, mwaka huu Kigali, Rwanda.

Baada ya kuivaa Rwanda, Stars itashuka tena dimbani Oktoba 18, mwaka huu kuumana na Sudan, katika pambano la marudiano la kusaka tiketi ya kufuzu fainali za mataifa ya Afrika kwa Wachezaji Wanaocheza Ligi za Ndani(Chan), utakaochezwa jijini Khartoum. 

Mchezo wa kwanza ulichezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, ambapo Stars ilibukali kichapo cha bao 1-0, hivyo ili kusonga mbele inahitaji ushindi wa mabao kuanzia mabao 2-0.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mgunda alisema wanataka kushinda mechi yao na  Rwanda, ili kujijengea hali ya kujiamini kabla ya kuivaa Sudan.

“Tumeanza mazoezi kujiandaa na mchezo dhidi ya Rwanda, sisi kama dawati la ufundi tumeamua kuutumia kama kipimo kuelekea mchezo wetu na Sudan, utaona hata kikosi kilichoitwa wachezaji wengi wanacheza ndani, hii ni kuonyesha kwamba lengo letu kuu ni kuunda mpango mkakati wa kufuzu.

“Tunajua Rwanda itakuwa kipimo kizuri kwetu kulingana na namna timu yao ilivyo, tumechagua tucheze ugenini ili kuwapunguzia presha wachezaji wetu, mkakati wa ushindi dhidi ya Sudan unaanzia Rwanda, kila kitu kinachukuliwa kwa uzito wa juu, lengo likiwa kupindua matokeo,” alisema Mgunda ambaye pia ni kocha wa Coastal Union inyoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles