28.3 C
Dar es Salaam
Saturday, November 26, 2022

Contact us: [email protected]

Puma kuuza mafuta kwa kadi ya Airtel Money

MENEJA Mkuu wa Puma Energy Tanzania,  Philippe Corsaletti (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (kulia),  wakiasini  mkataba wa makubaliano ya uuzaji wa mafuta kwa kutumia kadi ya Airtel Money Tap Tap , Hafla hiyo ilifanyika katika kituo cha Mafuta cha Puma Oysterbay jijini Dar es salaam juzi.
MENEJA Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso (kulia), wakiasini mkataba wa makubaliano ya uuzaji wa mafuta kwa kutumia kadi ya Airtel Money Tap Tap , Hafla hiyo ilifanyika katika kituo cha Mafuta cha Puma Oysterbay jijini Dar es salaam juzi.

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM

KAMPUNI ya mafuta ya Puma imezindua mfumo maalumu wa kununua mafuta kwa kutumia huduma mpya ijulikanayo kama ‘Airtel Money Tap Tap’ ambayo humwezesha kupata huduma hiyo katika kituo chochote nchini.

Akizungumza katika uzinduzi huo juzi Dar es Salaam, Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Philippe Corsaletti, alisema wana jukumu la kuhakikisha huduma wanazozitoa kwa ajili ya Watanzania zinakuwa salama wakati wote, ikiwa ni sehemu ya kuunga  mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano za kuhamasisha kutumia njia za kieletroniki kwenye malipo ya fedha.

Alisema kadi hiyo itamwezesha mteja pindi anapotaka kununua mafuta kwa kutumia  kadi ya Airtel badala ya kutoa fedha taslimu akiwa kituo cha mafuta.

Alisema wanahisi kwamba wanawajibu wa kufanya huduma zao kwa  usalama, zenye ufanisi na rahisi zaidi kwa wateja wao na kufafanua ni  hatari kubeba fedha wakati wote maana ni rahisi kuhatarisha maisha.

Aidha, alisema ili kuhakikisha jamii ya Watanzania inakuwa salama wakati  wote, kuna haja ya kuwa na huduma hiyo ambayo  itamuwezesha anayehitaji kununua mafuta kwenye vituo vya Puma  vilivyopo maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam wanatumia kadi za Airtel  kununua mafuta.

“Milango yetu iko wazi kwa ajili ya kuendelea kuboresha huduma zetu na tunaweza kufanya jambo lolote  ili kuhakikisha jamii yetu  inakuwa  salama wakati wote. Hivyo, kuna umuhimu wa kuwa na matumizi ya kadi ya Airtel katika kununua mafuta kwenye vituo vyetu vya  Puma.

“Kadi hii imeundwa kwa namna ambayo wakati wa kutumika kufanya malipo, hupunguza fedha kwa kiasi cha malipo kutoka katika akaunti  ya Airtel Money ya mnunuzi kwenda kwenye akaunti  ya muuzaji. Kadi hii itakuwa inauzwa kwa bei ya Shilingi 2, 000 kwenye vituo vyote vya Puma Dar es Salaam na maduka yote ya Airtel Tanzania,” alisema.

Alitumia nafasi hiyo kueleza kuwa Puma Tanzania ina jumla ya vituo 46  nchini kote na kwa kuanza, vituo vyote vya Dar es Salaam vitakua  vinatoa huduma hiyo na vilivyosalia vitaunganishwa kuanzia mapema mwakani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,558FollowersFollow
557,000SubscribersSubscribe

Latest Articles