23.4 C
Dar es Salaam
Sunday, May 29, 2022

PROFESA JAY aipeleka ‘Mwanalizombe’ Mikumi

JAYNA CHRISTOPHER MSEKENA

MSANII na Mbunge wa Jimbo la Mikumi, Joseph Haule ‘Profesa Jay’, amesema ana mpango wa kuihamishia studio ya Mwanalizombe kwenye jimbo lake ili aweze kutekeleza ahadi ya kuinua sanaa. Akizungumza na MTANZANIA, Profesa Jay alisema kuwa moja ya ahadi alizowaahidi

wakazi wa Mikumi kwenye kampeni zake ni kuibua vipaji vipya ndiyo maana ameamua kuihamishia studio hiyo huko ili aweze kutekeleza ahadi hiyo.

“Mikumi kuna vipaji vingi vya muziki lakini hakuna aliyeweza kuviibua kwa miaka mingi, ila mimi nikiwa kama Mbunge wao nitatekeleza ahadi hii kwa kuihamishia studio yangu Mikumi ili wasanii chipukizi waweze kufanya kazi zao,” alisema Profesa Jay.

Mwanalizombe ni studio inayomilikiwa na msanii huyo ipo maeneo ya Mbezi Luis, jijini Dar es salaam na imeshatoa nyimbo kali kama Makamanda wimbo wa Sugu, Tatu Chafu na Kipi Sijasikia chini ya mtayarishaji Villy.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,712FollowersFollow
542,000SubscribersSubscribe

Latest Articles