‘Ipo Siku’ yapakuliwa zaidi Mkito

0
1095

mtanzania kila siku safiSiah.inddNA CHRISTOPHER MSEKENA
NYOTA wa muziki wa injili nchini, Goodluck Gozbert, amewashukuru mashabiki kwa kupakuwa wimbo wake unaoitwa Ipo Siku kwenye tovuti ya Mkito inayojihusisha na kuuza nyimbo za wasanii mbalimbali.
Akizungumza na MTANZANIA, Goodluck alisema kuwa hiyo ni
hatua nzuri kwake kwa sababu zipo nyimbo nyingi nzuri za Injili lakini mashabiki wameichagua yake
hivyo anawashukuru na anaomba waendelee kumuunga mkono.
“Wimbo wangu umeongoza kupakuliwa kuliko wimbo wowote
ule wa Injili, hii ni hatua nzuri na inanipa moyo wa kuendelea kufanya
kazi nzuri ili mashabiki wazidi kubarikiwa na huduma ya nyimbo zangu,” alisema Goodluck.
Kwenye tano bora, Goodluck aliingia na wasanii wengine ambao
ni Boni Mwaitege, Samawati Band, Miriam Lukindo na Jeniffer Mgendi

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here