25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Prof. Mkenda akanusha wananchi wa Rombo kuwa walevi

Na Upendo Mosha, Rombo

MBUNGE wa Rombo, mkoani Kilimanjaro, Profesa Adolf Mkenda, amekanusha uvumi wa wananchi wa wilaya hiyo kuwa walevi wa kupindukia na kwamba ni wachapakazi na wenye bidii za kushiriki katika shughuli za maendeleo.

Mkenda alitoa kauli hiyo jana, wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mbomai, kata ya Tarakea Motamburu, katika hafla ya ufunguzi wa mradi wa matundu 16 ya vyoo katika shule ya msingi Mbomai juu, wilayani humo.

Alisema kumekuwa na baadhi ya watu ambao wamekuwa wakiichafu wilaya hiyo kwamba inaongoza kwa kuwa na walevi wengi ambao hawana kazi jambo ambalo si sahihi na kwamba tatizo la ulevi uliopinduzikia lipo katika maeneo mengi ya nchi.

“Rombo ina mambo mengi mazuri lakini bahati nzuri tumepata watani wengi wanapenda kututania kwamba sisi ni walevi,unaenda kuwahoji watu kwenye vilabu vya pombe unafikiri baa wanapatikana watu gani? baa watu wanakunywa pombe, Rombo wananchi wanapenda maendeleo sio walevi,” amesema.

Alisema wananchi wa Wilaya hiyo wamekuwa na desturi ya kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo na kuchangia miradi ya maendeleo kama ujenzi wa vyoo vya shule, Zahanati na madarasa na kwamba jamii iliyoathirika kwa ulevi uliopinduzikia haiwezi kufanya shughuli hizo.

“Wananchi wa Rombo wanashiriki katika shughuli za maendeleo na sasa wameamua kuanza na ujenzi wa vyoo bora vya kisasa na kwa hapa Rombo wananchi wamejenga Zahanati 10 kwa nguvu zao na jasho lao sasa walevi na wezaje kufanya kazi Kama hizi?…tukubali watani watutanie lakini tusibweteke kuchapa kazi,” alisema Profesa Mkenda

Mbali hilo Profesa Mkenda ambaye pia ni Waziri wa Kilimo, alitoa rai kwa wananchi wa jimbo hilo kuendelea kuiunga mkono serikali kwa kuendelea kuchangia miradi mbalimbali ya maendeleo hatua ambayo itasaidia upatikanaji wa huduma muhimu katika maeneo yao.

“Endeleeni kuiunga mikono serikali kwa kuchangia miradi ya maendeleo na wale wanaoichafua picha ya Rombo kwamba ni ya walevi waje waone maendeleo na hakuna asiyejua kwamba warombo ni wajasiriamali wakubwa na wanamiliki biashara nyingi ndani na nje ya nchi,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles