33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

TRA yajipanga kufanyakazi Kidigital

Na Christina Gauluhanga, Mtanzania Digital

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema imejipanga kufanya kazi kwa weledi kwa kutumia zaidi mitandao ili kupunguza misongamano inayoweza kuchangia maambukizi ya ugonjwa wa Covid 19.

Hayo yamesemwa Septemba 3, 2021 jijini Dar es Salaam na Mkurungezi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi(TRA), Richard Kayombo wakati akifungua Mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari na wanachama wa Klabu ya waandishi wa habari Dar es Salaam (DCPC) yalioandaliwa na Mamlaka hiyo ili kuweza kufikisha elimu kwa wananchi kuhusu mabadiliko ya Sheria za Kodi kwa mwaka 2021.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo, akizungumza wakati wa semina kwa waandishi wa habari wanachama wa Dar es Salaam City Press Club (DCPC) kuhusu mabadiliko ya sheria za kodi kwa mwaka 2021.

Alisema TRA tayari imefanikiwa kupunguza misongamano kwa kuanzisha minada mitandaoni, utoaji risiti kwa njia ya kieletroniki na ulipaji kodi za majengo.

Amesema huduma kuhamia kwa njia ya kielektroniki itaongeza ufanisi na ushindani wa haki kwa washiriki ambapo kwa sasa utajumuisha nchi nzima tofauti na awali kufanyika Dar es Salaam peke yake

‘Wakati tukiendelea kupambana na janga hili la Corona hatutaki mambo mengine yasimame tutahakikisha tunaeendelea kukusanya kodi kama ilivyopangwa na Serikali,”alisema Kayombo.

Amesema pia TRA inafanya ushirikishaji katika maeneo mbalimbali ili kuwasaidia wananchi waweze kulipa Kodi kwa wakati pamoja na Mamlaka hiyo kukusanya kwa weledi ili kufikia lengo husika ili Shughuli za maendeleo ziweze kufanyika.

” Tumejipanga kuwatumikia wananchi katika kusimamia mapato na tumekuwa tukitoa elimu kwa walipata Kodi wetu kuhusu umuhimu wa kulipa Kodi na kujua haki zao kama walipa Kodi,”amesema Kayombo.

Amesema TRA imekuwa ikihusika zaidi na mapato ya Serikali kuu huku majukumu yao ya msingi ya kusimamia yakiwa ni pamoja na kuzingatia uwajibikaji, Weledi na Uhadilifu.

Amebainisha kuwa majukumu hayo yamekuwa yakisimamiwa kwa maagizo yaliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari wa Dar es Salaam (DCPC), Irene Mark akichangia mada wakati wa semina kwa waandishi wa habari wanachama wa Dar es Salaam City Press Club (DCPC) kuhusu mabadiliko ya sheria za kodi kwa mwaka 2021.

Naye, Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Dar salaam (DCPC), Irene Mark aliwataka wanahabari hao kuyazingatia Mafunzo waliyoyapata ili yaweze kutumika kuelimisha jamii katika masuala mazima ya tozo.

Amesema DCPC ilianzishwa mwaka 2003 ambapo imekuwa ikifanya mambo mbalimbali lengo kuu likiwa ni kuwaunganisha waandishi wa habari, kutafuta fursa na kujadili changamoto zinazowakabili.

Amewaasa wanachama hak kutumia vyema Mafunzo haya kwani yakitumika vizuri kwa wanahabari yatasaidia wananchi kutambua na kujua umuhimu wa kulipa Mapato,”amesema Irene

Aidha alitoa wito kwa wanahabari hao kujitokeza kupata chanjo ya virusi vya UVIKO 19 kama njia ya kujikinga na maradhi hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles