Prodyuza atuhumiwa kwa ubakaji

0
487

NA MANENO SELANYIKA

PRODYUZA na mmiliki wa studio ya muziki ya Smarts Records iliyopo Sala Sala, Gray Bosco (27), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni akikabiliwa na tuhuma za kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 15.

Mbele ya Hakimu Frank Moshi, Wakili wa Serikali, Ramadhani Mkimbu, alidai kwamba Gabriel alitenda kosa hilo Julai 18, mwaka jana, eneo la Mmbuyuni, wilayani hapo.

Mkimbu alieleza kwamba mtuhumiwa alifanya tendo hilo na kumsababishia maumivu makali msichana huyo wakati akitambua kuwa ni kinyume cha sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hata hivyo, mtuhumiwa alikana kosa hilo, lakini alishindwa kutimiza masharti ya dhamana hivyo akarudishwa rumande. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 25, mwaka huu.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here