21 C
Dar es Salaam
Friday, August 12, 2022

Polisi yakana kuwateka wasaidizi wa Mnyika; walishikiliwa kwa mahojiano

Benjamin Masese, Mwanza

Jeshi la Polisi mkoani Mwanza limesema hakuna  viongozi wa  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wala wasaidizi wa Katibu Mkuu wa chama hicho. John Mnyika waliotekwa mkoani humo isipokuwa walishikiliwa kwa mahojiano.

Amesema hatua hiyo ilikuja baada ya wananchi wa Kata ya Mahina kutoa taarifa kwamba si watu wema.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Desemba 30, Kamanda wa  Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro amesema taarifa zilizosambaa tangu juzi katika mitandao ya kijamii kwamba wanachama wa Chadema ambao ni wasaidizi wa Mnyika wametekwa si za kweli na kuwataka wananchi kuzipuuza.

“Viongozi waliokuwa wameshikiliwa na polisi ni Katibu wa Katibu Mkuu wa Chadema, Abdulkarim Muro (31) na dereva wa Mnyika, Said Haidani (30) na walikuwa mikononi kwa polisi tangu juzi saa 12 jioni baada ya raia wema kutoa taarifa polisi kwamba kuna watu wawili wanahisiwa si wema na wamekuwa wanaingia katika nyumba moja iliyopo karibu na Hoteli ya Paradise.

“Baada ya taarifa hizo polisi walifuatilia kwa haraka na kufanikiwa kuwakamata na walipotakiwa kutoa maelezo ya awali ya utambulisho waligoma na kulazimika kuwapeleka katika kituo kikuu cha kati, hivyo baada ya polisi kujiridhisha tumewachia na wanaendelea na shughuli zao,” amesema Muliro.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,504FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles