G. Nako aagana na ukapera

0
1157

BRIGHITER MASAKI-DAR ES SALAAM

MSANII wa muziki wa hip hop nchini, kutoka kundi la Weusi, George Mdeme ‘G Nako’ ameagana na ukapera baada ya usiku wa kuamkia juzi kufunga ndoa na mzazi mwenzake anayefahamika kwa jina la Yasinta.

Mkali huyo amefunga katika kanisa Katoliki St Peter na baadae kufanyika sherehe katika hoteli ya Golden Tulip, iliyopo jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza na MTANZANIA jana, G. Nako alisema anamshukuru Mungu kwa kufanikisha jambo hilo muhimu katika maisha ya binadamu.

“Namshukuru Mungu kwa kukamirisha jambo hili, sasa ni mume sahihi wa Yasinta, nampenda mke wangu na Mungu atujalie tuzidi kupendana na tuwe wavumilivu,”alisema G. Nako.

Mastaa mbalimbali walijitokeza kwenye harusi hiyo kama vile Juma Jux, Nikki wa Pili, Joh Makini na wengi wengi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here