27.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 4, 2023

Contact us: [email protected]

Polisi wajinoa kukabili Ukuta  

POLISIEDITHA KARLO, KAGERA NA PETER MAKUNGA, BUKOMBE

JESHI la Polisi limejipanga kukabiliana na Operesheni Ukuta, huku viongozi mbalimbali wa Chadema wakikamatwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro, alisema kwamba maandamano hayo hayatafanyika na jeshi la polisi limejipanga kuyazuia maandamano hayo.

Kamanda Sirro alisema kuwa hakuna habari ya Ukuta na hakuna mtu atakayethubutu kuingia barabarani kutokana na jeshi lilivyojipanga kuhakikisha wananchi wanafanya shughuli zao bila kuingiliwa na kitu chochote.

Alisema utaratibu wa kufanya mikutano ya siasa umeelezwa, hivyo kufanya bila kufuata utaratibu hakutaruhusiwa.

Kamishna Sirro alisema watu wanaotaka kutumia siasa katika kuvunja amani hawatakuwa na nafasi na kwamba watadhibitiwa na jeshi hilo.

 

BUKOBA

Taharuki kubwa imejitokeza jana katika Manispaa ya Bukoba kufuatia milipuko mikubwa ya mabomu yaliyokuwa yakipigwa na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU).

Milipuko hiyo ya mabomu ilianza kusikika saa nne asubuhi maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Bukoba.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Agustino Ollomi, alisema kuwa wapo katika mazoezi ya kawaida.

 

VIONGOZI WAKAMATWA

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Geita, Upendo Peneza (Chadema) pamoja na Ofisa wa Chadema Kanda ya Ziwa Victoria, Tungaraza Njugu, wamekamatwa jana wilayani Bukombe mkoani Geita.

Viongozi hao wamekamatwa wakati wakiwa kwenye vikao vya chama pamoja na wanachama wengine 12, wakituhumiwa kupanga maandamano ya Ukuta.

Katika maeneo mbalimbali ya nchi hivi sasa, askari polisi wamekuwa wakiendesha mazoezi yenye lengo la kujipanga kukabiliana na Ukuta.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles