30.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 19, 2021

POLISI DAR WAVUNJA MKUTANO

  • Uliitishwa na vijana kujadili haki za binadamu

Na ANDREW MSECHU, DAR ES SAALAM


JESHI la Polisi jana lilivunja mkutano ulioandaliwa na taasisi za vijana kuzungumzia mwenendo mbovu wa haki za binadamu na uvunjwahji wa haki za msingi katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Mkutano huo uliotarajiwa kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Landmark, Ubungo kuanzia saa tano asubuhi jana, ulikwama kuendelea baada ya kuvamiwa na polisi huku waandaaji wakitimua mbio kwa hofu ya kutiwa nguvuni.

MTANZANIA lilikuwapo eneo la mkutano huo kuanzia saa 4 asubuhi na liliwashuhudia washiriki kutoka taasisi za Umoja wa Kizazi cha Kuhoji Tanzania (UTG) na Kamati ya Mshikamano Kati ya Vijana wa Tanzania na Sahara Magharibi (TASSC).

Wakiwa ndani ya ukumbi, ghafla aliingia ofisa mmoja wa polisi aliyekuwa amevalia sareza jeshi hilo na kujitambulisha kwa mlinzi kwamba naye ni mshiriki.

Baada ya kupewa maelezo, ofisa huyo ambaye jina lake halikuweza kupatikana alimweleza mlinzi huyo kuwa hawezi kuingia kutokana na sare zake za kazi na kuita askari wengine waliovalia kiraia ambapo alitoka nje na baada ya muda waliingia askari polisi waliokuwa na silaha za moto kwenye ukumbi wa mkutano.

Hatua hiyo ilizua taharuki miongoni mwa wanahabari na waandaaji wa mkutano huo, baada ya kubaini kuzingirwa na askari kanzu waliovaa kiraia huku askari wenye silaha wakizingira pia eneo hilo na hivyo kuwalazimu waandaaji na wanahabari kila mmoja kuanza kutawanyika ki vyake.

Akizungumzia tukio hilo, Mratibu wa Uhusiano kwa Umma wa Taasisi ya Tanzania Sahrawi Solidarity Committee  (TASSC), Noel Shao alisema walilazimika kusitisha kutoa tamko lao ukumbini hapo baada ya kuhofia usalama kutokana na kuzingirwa na polisi.

“Polisi wenye sare na silaha na askari kanzu wakiwa ndani ya gari zisizo pungua nne za polisi ziliendelea kupiga kambi kwenye Hoteli ya Land Mark kwa zaidi ya saa moja kuhakikisha hatutoi tamko. Hata hivyo, tutaendelea kuwasiliana na umma kupitia njia nyingine za mawasiliano ili kupaza sauti zetu dhidi ya ukandamizwaji wa demokrasia na haki za binadamu,” alisema.

MTANZANIA lilipomtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Jumanne Muliro alisema hajui lolote wala hana taarifa za kutawanywa kwa mkutano huo.

Baada ya saa chache, waandaaji hao walitoa taarifa yao ambayo MTANZANIA inayo nakala yake ikiwa imeorozesha waandaaji kuwa ni Taasisi za Umoja wa Kizazi cha Kuhoji Tanzania (UTG), Kamati ya Mshikamano Kati ya Tanzania na Sahara Magharibi (TASSC) na Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP).

Kwa pamoja, mitandao hiyo kupitia kwa mratibu wao, Shao walieleza kuwa wanaharakati wa haki za binadamu, asasi za kiraia na wananchi karibu nchi zote za Afrika Mashariki  wamekuwa wakishughulikiwa ili kuhakikisha baadhi ya tawala za kidekteta zinatawala bila kikwazo……………

 

KWA HABARI KAMILI,

JIPATIE NAKALA YAKO YA GAZETI LA MTANZANIA SASA!!

 

 

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
156,848FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles