28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

Pluijm: Tunaandaa dozi ya Mgambo Bagamoyo

pluijmNA JENNIFER ULLEMBO, DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa Yanga, Hans Van der Pluijm, amesema watahakikisha wanatumia kambi ya Bagamoyo kuandaa dozi nzito itakayoacha historia katika mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya Mgambo Shooting Jumamosi hii jijini Tanga.

Kikosi hicho ambacho kiliondoka jana jioni kuelekea Bagamoyo kwa ajili ya kambi ya siku tatu, kinatarajiwa kuelekea mkoani Tanga siku ya Alhamisi kwa ajili ya mchezo huo wa ligi utakaochezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Pluijm alisema kambi hiyo ni ya muda mfupi, lakini itazaa matunda mazuri katika mchezo huo waliokuwa wakiusubiri kwa hamu.

“Wengi wanaweza jiuliza kwanini tunaweka kambi ikiwa siku zilizosalia kabla ya mechi ni chache, hilo sisi halitupi shida, ninachotambua kikosi changu kinaingia kambini.

“Tutahakikisha tunaacha histori mkoani Tanga, hata tutakapokutana nao tena tushuke dimbani kwa heshima na kumbukumbu nzuri,” alisema Pluijm.

Mholanzi huyo alieleza kuwa wakiwa mjini Bagamoyo, kikosi chake kitakuwa kikifanya mazoezi mara mbili kwa siku na kwa kuhakikisha hilo linafanikiwa, zoezi hilo lilianza jana.

Timu hiyo jana jioni ilifanya mazoezi yake ya mwisho katika viwanja vya Boko Veterani, kabla ya kuelekea Bagamoyo ambapo itaweka kambi na kuunganisha safari ya Tanga.

Mechi za Ligi Kuu zinatarajiwa kuendelea Desemba 12 katika viwanja mbalimbali hapa nchini, ambapo Yanga inashikilia nafasi ya pili katika msimamo wa ligi ikiwa na jumla ya pointi 23.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles