24.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 31, 2023

Contact us: [email protected]

Miss Albino Arusha kupatikana Desemba 18

MISS ALBINONA GEORGE KAYALA

SHINDANO la kumsaka mrembo wa watu wenye ulemavu wa ngozi ‘Miss Albino Tanzania’ linalofanywa kikanda linaendelea Desemba 18, mwaka huu katika Jiji la Arusha.

Shindano hilo linatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa Triple A huko Arusha ambapo wasichana kadhaa watashindanishwa kumpata Miss Albino Kanda ya Kaskazini.

Mratibu wa shindano hilo, Alexander Matowo, alisema shindano hilo litafanyika kanda zote kisha washindi wa kila kanda watashindanishwa kwa ajili ya kumpata Miss Albino Tanzania.

Tayari mshindi wa Kanda ya Pwani ameshapatikana ni Priscilla Samweli (22) ambaye ni mkazi wa Chanika jijini Dar es Salaam.

Shindano hilo limeandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Save Vulnerable Foundation (SVF) na lengo lake ni kuibua na kutambua vipaji vya albino, kujenga ujasiri, kuwawezesha kufikia malengo yao, kuwajenga kiafya, kiuchumi na kielimu pia kupata Sh milioni 90 kwa ajili ya ujenzi wa maktaba na jiko katika kituo cha walemavu kilichopo Buhangija Mkoa wa Shinyanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,207FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles