23.3 C
Dar es Salaam
Sunday, October 6, 2024

Contact us: [email protected]

PLUIJM ATUMA SALAMU AZAM

NA RAMADHAN HASSAN-DODOMA

KOCHA Mkuu wa Kikosi cha Singida United, Hans van der Pluijm, mara baada ya timu yake  kupata ushindi juzi dhidi ya Kagera Sugar, amesema dozi sasa inahamia kwa Azam ya Dar es Salaam.

Singida United iliibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wake wa juzi dhidi ya Kagera Sugar, katika Uwanja wa Jamhuri, mjini hapa, bao lililofungwa na Tafadzwa Kutinyu.

Kutokana na ushindi huo, Singida United sasa inashika nafasi ya tatu baada ya kufikisha pointi tisa katika michezo minne iliyocheza mpaka sasa.

Timu hiyo ilifungua ligi kwa kufungwa mabao 2-1 na Mwadui, kisha kuifunga Mbao mabao 2-1, baadaye wakawafunga Stand United bao 1-0 na juzi kuibamiza Kagera Sugar kwa bao 1-0.

Pluijim huo ulikuwa mchezo wake wa kwanza kukaa kwenye benchi, baada ya kumaliza adhabu aliyopewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kosa la kuwatolea lugha chafu waamuzi akiwa kocha wa Yanga katika msimu uliopita wa Ligi hiyo.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo, Pluijm alisema mara baada ya kupata ushindi timu yake inajipanga kwa ajili ya mchezo unaofuata dhidi ya Azam, unaotarajiwa kufanyika Jumamosi katika Uwanja wa Jamhuri, mjini hapa.

“Unapomaliza mchezo mmoja mara moja unaanza maandalizi ya mchezo unaofuata, tutaendelea kuwepo hapa Dodoma tukijiandaa na mchezo unaofuata dhidi ya Azam, naamini tutapata ushindi,” alisema.

Akiuzungumzia mchezo dhidi ya Kagera Sugar, Pluijm aliwalaumu wachezaji wake kwa kupoteza nafasi nyingi, huku akidai wamepoteza nafasi zaidi ya tano.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles