29.8 C
Dar es Salaam
Monday, October 7, 2024

Contact us: [email protected]

CAVANI AKATAA BIL 2 KUMWACHIA PENALTI NEYMAR

PARIS, UFARANSA

MSHAMBULIAJI wa klabu ya PSG, Edinson Cavani, ameitolea nje ofa ya klabu hiyo ya Euro milioni moja, zaidi ya Sh bilioni mbili za Kitanzania ili amwachie Neymar kupiga mipira ya penalti.

Wiki moja iliyopita, Cavani alirushiana maneno na Neymar katika kuwania kupiga penalti kwenye mchezo dhidi ya Lyon, huku PSG ikifanikiwa kushinda mabao 2-0 kwenye michuano ya Ligi Kuu nchini Urafansa.

Neymar amejiunga na klabu hiyo katika kipindi hiki cha majira ya joto akitokea Barcelona na kumkuta Cavani akiwa mpigaji mkuu wa penalti na mipira ya adhabu karibu na eneo la 18, lakini baada ya Neymar kujiunga na kikosi hicho, akawa anang’ang’ania kupiga yeye kinyume na utaratibu.

Wawili hao wakaingia kwenye mgogoro wa kurushiana maneno ndani ya uwanja na kwenye chumba cha kubadilishia nguo jambo lililowashangaza mashabiki na wadau wengi wa soka.

Kutokana na hali hiyo, PSG wakaamua kuweka mezani kitita cha bilioni 2 na 629,420,000 ili kumtaka Cavani aache kupiga mipira ya penalti na kumwachia nafasi hiyo Neymar ambaye amesajiliwa kwa kiasi kikubwa duniani kuliko mchezaji yeyote, pauni milioni 198.

Hata hivyo, kwa mujibu wa mitandao ya soka nchini Hispania, ikiwamo na El Pais, imeandika kwamba Cavani amepewa ofa hiyo lakini amekataa.

Rais wa klabu hiyo, Nasser Al-Khelaifi, alikutana na Cavani wiki iliyopita na kujaribu kufikia makubaliano baada ya kuona kwamba walipishana kauli na Neymar mapema Septemba 18.

Lakini mchezaji huyo amesisitiza kuwa ataendelea kuwa mpigaji wao wa penalti kama ilivyo kawaida na anafurahia nafasi hiyo pamoja na ile ya unahodha namba tatu wa timu hiyo.

Washambuliaji hao wawili wamekuwa ni wachezaji walioifanya PSG kutumia fedha nyingi kuwasajili, huku ikiwa imetumika pauni milioni 253 kukamilisha usajili wao kwa nyakati tofauti, lakini kwa kipindi hiki kifupi tayari wameonekana hawana maelewano mazuri.

Hata hivyo, inasemekana kuwa wachezaji wengi wa klabu hiyo wanaonekana kumpa nguvu Cavani kuwa mpigaji wao wa penalti na ndiyo maana amekataa ofa hiyo kutoka kwa uongozi wa klabu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles