PINDA ASEMA WAPINZANI WATAPATA TAABU SANA UKONGA

0
984
WAZIRI Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda

Na AGATHA CHARLES            |                   


WAZIRI Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda, amesema anajisikia raha kuwa mwanachama wa CCM na sio mwanasiasa wa kusimama jukwaani kulalamika na kunung’unika.

Pinda alitoa kauli hiyo jana wakati wa uzinduzi wa kampeni za CCM katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Ukonga katika viwanja vya Kivule Shule ya Msingi.

“Najisikia raha kuwa CCM, sio unasimama jukwaani kulalamika na kunung’unika, ukigeuka huku wamekula mweleka, hapo ndio nakumbuka ule msemo watapata taabu sana sio wapigwe tu. Kwa sasa wajitafakari sio kusema wamenunuliwa,” alisema Pinda.

Aliongeza kwa kusema msingi wa CCM ni mabalozi na ndio walioshikilia chama hicho kwa sababu wanawajua watu wao hivyo, aliwataka viongozi kukutana nao.

Pinda alisema alipata nafasi ya kuzungumza na mgombea wa CCM, Mwita Waitara kujua undani wa ushindi wake wakati akiwa Chadema, na alimjibu kwamba ulitokana na kupigiwa kura na watu wa chama hicho tawala.

Alisema jimbo hilo lina mitaa 70 na kati ya hiyo 59 ilikuwa ya CCM, minane ya Chadema na mitatu ya CUF ambayo katika hali ya kawaida Waitara asingeshinda.

Pinda alisema katika mazungumzo hayo na Waitara, pia alieleza kuhusu …

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here