24.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

Pinda apiga marufuku wenye viti wa vijiji na mitaa kuuza maeneo

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Geophrey Pinda amepiga marufuku wenyeviti wa vijiji kuuza viwanja na mashamba kwakuwa wamekuwa ni chanzo cha migogoro mingi ya ardhi.

Pinda amesema hayo wakati alipofanya ziara ya katika kijiji cha Kitwai B wilayani Simanjiro mkoa wa Manyara ili kukutana na wananchi wenye mgogoro wa mpaka kati ya wilaya ya Kilindi mkoa wa Tanga na Simanjiro mkoa wa Manyara.

“Hakuna mgogoro wowote wa mpaka huku, tatizo liliopo hapa ni baadhi ya viongozi hususan wenyeviti wa vijiji kuuza maeneo kiholela holela kwa watu wanao wajua wao na ndio maana kuanzia leo ni marufuku uuzaji wa maeneo chini ya mamlaka ya wenyeviti wa vijiji sababu ndio chanzo kikubwa cha migogoro,” amesema Pinda.

Aidha, Pinda amemuomba Waziri wa TAMISEMI kumsimamisha mwenyekiti wa Kijiji cha Gitu wilaya Kilindi mkoani Tanga kwakuwa ndio chanzo kikubwa cha migogoro ya ardhi ya eneo hilo kwani amekuwa akiuza ardhi bila kufuata taratibu za mipango ya matumizi ya ardhi.

Katika Hatua nyingine Pinda ameelekeza kuondolewa Mpima Ardhi Msaidizi wa mji wa Merelani kwa kuwasumbua wananchi na kukaidi maelekezo ya viongozi wa Serikali katika kusimamia masuala ya upimaji na umilikishaji ardhi.

“Yule Afisa Ardhi wa Merelani anasumbua wananchi wa Merelani, huyu naondoka nae mimi kwenda Dodoma sababu ameshindwa kufanya kazi yake na amekuwa akikaidi maelekezo mbalimbali anayopewa na viongozi wake wa Serikali kuu na Wilaya,” alisema Pinda.

Pinda amesisitiza kuwa utaratibu wa umilikishaji wa ardhi za vijiji unawataja wakurugenzi wa Halmashauri ambao ndio wasimamizi wa utaratibu wa umilikishaji wa ardhi za vijiji na sio wenyeviti wa vijiji japo ardhi hiyo inamilikiwa na kijiji.

Kwa upande wa mgogoro wa mpaka kati ya Wilaya ya Kilindi na Simanjoro Naibu Waziri Pinda amesema hakuna mgogoro wowote wa wilaya hizo bali ni baadhi ya viongozi wa vijiji kuuza maeneo yaliyowekewa mipango ya matumizi ya ardhi kijolela.

Pinda amewataka wakazi hao kuishi kwa amani na upendo bila kugombana na kuepuka ugomvi wa mipaka mpaka yatakapokuja maelekezo rasmi ya Serikali ya usimamizi wa eneo hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles