25.8 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania yathibitishwa kuwa mjumbe wa Baraza Tendaji la UNWTO

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Tanzania imethibitishwa na Mkutano Mkuu wa 25 wa Shirika la Utalii Duniani (UNWTO) kuwa Mjumbe wa Baraza Tendaji la Shirika hilo kwa kuchaguliwa bila kupingwa na nchi wanachama wa Shirika la UNWTO.

Uchaguzi huo umefanyika Oktoba 19, 2023 jijini Samarkand, Uzbekistan ambako Mkutano Mkuu wa 25 wa UNWTO unaendelea.

Kupitia nafasi hiyo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki ataiwakilisha Afrika kwa kipindi cha Miaka minne (2023 – 2027) katika mikutano muhimu ya Baraza hilo itayokuwa ikifanyika mara mbili (2) kwa mwaka.

Akizungumza baada ya Tanzania kuthibitishwa katika nafasi hiyo, Kairuki ameeleza kuwa nafasi hiyo ni muhimu katika kukuza na kutangaza utalii wa Tanzania na Afrika kwa ujumla kwa kuwa Baraza hilo ni chombo muhimu kinacho simamia Mipango na Bajeti ya Shirika pamoja na utekelezaji wake.

Aidha, Waziri Kairuki ameongeza kuwa, kupitia nafasi hii, Tanzania itashiriki kupeleka agenda muhimu zenye maslahi mapana ya maendeleo ya utalii wa Bara la Afrika na Duniani kwa ujumla.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles