24.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

Makondakta nao kusajiliwa LATRA

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

BAADA ya kufanikiwa kwa madereva, Mamlaka ya Udhibidi Usafiri Ardhini (LATRA), inatarajia kuanza usajili wa watoa huduma na makondakta wa mabasi ikiwa ni hatua ya kuongeza ufanisi wa utendaji kazi katika kuwahudumia abiria.

Mafunzo kwa wahudumu yanakusudiwa kuanza kabla ya mwisho mwa mwezi huu wa Oktoba, 2023, lengo likiwa ni kuhakikisha wahudumu wa vyombo vinavyodhibitiwa wanafahamu sheria, kanuni na taratibu za usafiri ardhini.

Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, CPA Habibu Suluo anasema LATRA inapenda inapenda kuona wahudumu wakiwa nadhifu, wanaheshimu na kuheshimika kwa kazi wanayoifanya pamoja na kuwajengea uwezo wa kutoa huduma bora kwa abiria.

Sulue anasema katika kufanikisha azima yake, LATRA watatumia mfumo walioutumia kusajili madereva ili kuwasajili watoa huduma hao na kwamba kabla ya kusajiliwa watapewa mtihani wa kupima uelewa na uwezo wao katika maeneo muhimu yanayogusa meneo ya kazi zao.

“Sheria inataka tuwasajili wahudumu, unajua kwenye masuala haya ya usafiri wahudumu hawa makondakta  nao wana mchango mkubwa pale unapokwenda kukata tiketi,” anasema Sule  kwenye mkutano wa LATRA na Wahariri wa Vyombo vya Habari.

Mkutano huo uliofanyika Oktoba 19, 2023 jijini Dar es Salaam ni mwendelezo wa mikutano ya taasisi za umma na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari inayoratibiwa na ofisi ya Msajili wa Hazina.

Sule anaeleza kuwa hadi Septemba 30,2023, LATRA walishasajili madereva 17,990 na kuwaingiza katika kanzidata ya mamlaka, huku madereva 1,617 wakiwa tayari wamethibitishwa baada ya kufaulu mtihani.

“Madereva 645 wamesajiliwa kwenye mfumo wa kufuatilia mwenendo wa mabasi na kupewa kitufe maalumu cha utambulisho kiliunganishwa na mfumo wa VTS,”anasema Sule. Anasema umuhumu wa kitufe hicho ni kurahisisha utambuzi wa dereva anayeendesha gari kwa wakati husika kupitia mfumo  huo ambapo inakuwa ngumu kumpa dereva mwingine asiyesajiliwa.

Mkurugenzi huyo amesema  madereva wote waliopewa vibali vya safari za usiku wamepewa kifaa hicho na hata akibadilishana na mwenzake anajulikana, hali iliyosaidia kupunguza ajali.

Katika hatua nyingine Sule amesema wamebaini mchezo mchafu unaofanywa na watoa huduma ya usafiri wa kukodi  kupitia mtandao  ili kukwepa  kodi au kumfanya abiria kutoa kiasi kikubwa cha nauli.

Amesema  pamoja na kuwaita wahusika na kuwaonya lakini suala hilo wanaendelea  kulifanyia kazi ili kuweka mfumo thabiti wa kukabiliana na vitendo hivyo.

“Hizi teksi mtandao zinapobeba  abiria wao tunaona, umelipa shilingi ngapi tunaona, shida ambayo ipo wanaambia watu ‘cancel’ safari, ina maana serikali inapoteza mapato,” anaeleza.

Kwa mijibu wa LATRA, huduma hiyo iliyoanza mwaka 2017 nchini, hadi sasa jumla ya  kampuni 15 zimepatiwa leseni na mamlaka  imepanga viwango vya nauli elekezi na magari yapatiwa leseni  kutoa huduma hiyo katika mwaka 2022/23 ni 3,523 ikiwa ni ongezeko la asilimia 16.9.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles