Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akipokea zawadi ya picha kutoka kwa Ahmed Salim mtoto wa Dkt. Salim Ahmed Salim ambaye alikabidhiwa na Serikali ya China ikiwa ni ishara ya kuutambua mchango wa Dk. Salim ulioiwezesha China kurejesha kiti cha Kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwaka 1971.Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (kushoto) akizungumza na Ahmed Salim (katikati) mtoto wa Dk. Salim Ahmed Salim ambaye alifika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kumkabidhi zawadi ya picha iliyotolewa na Serikali ya China ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa Dk. Salim ulioiwezesha China kurejesha kiti cha Kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwaka 1971.