28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Petr Cech kuikosa Tottenham kesho

Petr CechLONDON, ENGLAND
MLINDA mlango wa Arsenal, Petr Cech, ataukosa mchezo wa Ligi Kuu kesho dhidi ya Tottenham kwenye Uwanja wa White Hart Lane.
Mchezaji huyo anasumbuliwa na maumivu ya misuli ambayo aliyapata juzi kwenye mchezo dhidi ya Swasea City, ambapo Arsenal ilipokea kichapo cha mabao 2-1 nyumbani kwenye Uwanja wa Emirates.
Kocha wa klabu hiyo Arsene Wenger, amekiri kumkosa mchezaji huyo katika mchezo wa kesho na nafasi yake ikitarajiwa kuchukuliwa na David Ospina.
“Matatizo ambayo ameyapata Cech si makubwa sana, lakini hawezi kucheza mchezo wa kesho, nafasi yake itazibwa na Ospina na wala hakuna wasi wasi kwa hilo.
“Sijui atakuwa nje ya uwanja kwa muda gani, lakini tunatarajia kumuona kipindi kifupi kijacho,” alisema Wenger.
Hata hivyo, Wenger anaamini kuwa kikosi chake bado kina wachezaji wazuri ambao wanaweza kufanya vizuri katika mchezo huo wa kesho.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles