24.7 C
Dar es Salaam
Saturday, April 13, 2024

Contact us: [email protected]

Van Gaal: Furaha imeanza Man United

Manchester United v Manchester City, Barclays Premier League Football, Old Trafford, Britain - 12 Apr 2015MANCHESTER, ENGLAND
BAADA ya Manchester United kufanikiwa kushinda bao 1-0 dhidi ya Watford kwenye Uwanja wa Old Trafford, kocha Van Gaal amedai kwamba furaha imeanza kurudi katika klabu hiyo kutokana na ushindi wanaoupata.
Katika mchezo huo wa juzi, japokuwa United walikuwa nyumbani lakini hali ilikuwa ngumu kutafuta bao hilo ambalo lilifungwa katika dakika ya 83 kwa mkwaju wa adhabu ambao ulipigwa na Juan Mata.
Van Gaal anaamini timu yake kwa sasa ipo katika kiwango kizuri ambapo ni mchezo wa pili mfululizo ikishinda kwenye uwanja wa nyumbani, ambapo wiki iliopita ikishinda mabao 3-2 dhidi ya Arsenal.
“Kwa sasa timu inapambana kwa ajili ya kutafuta ushindi katika kila mchezo mbele yake, kikubwa ni kucheza kwenye kiwango ambacho tulikionesha kwenye mchezo dhidi ya Arsenal, kwa kuwa tulipambana hatua ya mwanzo hadi mwisho.
“Ninaamini vijana wadogo wanaonesha uwezo wao kwa ajili ya kujitafutia namba, kwa sasa kila mchezo tukimaliza wachezaji wanakuwa na sura zenye furaha kubwa huku wakicheka, hali hii itawafanya wachezaji kurudi katika kiwango chao,” alisema Van Gaal.
Manchester United kwa sasa inashika nafasi ya tano katika msimamo wa Ligi huku ikiwa na alama 47 sawa na wapinzani wao Manchester City ambao wanashika nafasi ya nne.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles