32.2 C
Dar es Salaam
Thursday, February 2, 2023

Contact us: [email protected]

Michel Platini akata rufaa

Michel PlatiniZURICH, USWISI
ALIYEKUWA Rais wa Vyama vya Soka barani Ulaya, Michel Platini, amekata rufaa katika mahakama ya nchini Uswisi kufuatia kifungo chake cha kutojihusisha na michezo kwa miaka sita.
Kiongozi huyo alisimamishwa kazi kutokana na kashfa ya kupokea rushwa kutoka kwa aliyekuwa Rais wa Shirikisho la soka Duniani, Sepp Blatter ya dola milioni 2.
Kufungiwa kwa rais huyo kulimfanya akose nafasi ya kugombea urais wa shirikisho hilo ambao ulifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita na Gianni Infantino kuibuka mshindi.
Platini ameiomba mahakama hiyo ya Uswisi kutupilia mbali hukumu hiyo ya miaka sita iliyopunguzwa hivi karibuni na FIFA kutoka miaka 8.
“Bado ninaamini kuna haki yangu na ndio maana ninafuatilia hadi hatua za mwisho, nimekata rufaa nyingine kwenye mahakama ya Uswisi ninaamini kila kitu kitakuwa sawa mapema iwezekanavyo,” alisema Platini.
Hata hivyo, Platini ameitaka FIFA itoe uamuzi mapema kabla ya michuano ya ubingwa wa Ulaya nchini Ufaransa inayotarajia kuanza Juni mwaka huu.
Platini alikanusha kupokea rushwa na kudai kwamba fedha hizo za dola milioni 2 alizopewa na mkuu wa zamani wa FIFA, zilikuwa ni malipo ya kazi ya ushauri aliotoa miaka tisa iliyopita na zilikuwa halali kutokana na makubaliano yao.
Sepp Blatter anakabiliwa na marufuku ya miaka sita kuhusu suala lilo hilo anatarajiwa pia kuwasilisha kesi yake mbele ya mahakama hiyo inayotoa uamuzi wa mwisho kuhusu mizozo aina hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles