28.1 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

Perez adai Benzema amemsahaulisha Ronaldo

MADRID, Hispania

RAIS wa Real Madrid, Florentino Perez, amemshukuru Karim Benzema kwa kuendelea kukipiga klabuni hapo, akisema amemsahaulisha kuondoka kwa Cristiano Ronaldo.

Benzema amekuwa straika tegemeo zaidi kikosini baada ya pacha wake, Ronaldo, kutimkia Juventus ya Italia wakati wa usajili wa kiangazi, mwaka jana.

Hivi sasa, Perez amekuwa na mazungumzo ya mara kwa mara na Benzema, akisema amekuwa akipitia nyakati ngumu lakini bado ameendelea kukomaa Santiago Bernabeu.

Nyota huyo ameshafunga mabao tisa na kutoa asisti mbili msimu huu wa Ligi Kuu ya Hispania ‘La Liga’.

“Najisikia furaha, licha ya kuondoka Cristiano Ronaldo, aliyekuwa akitufungia mabao kila kukicha.

“Mwazoni mwa msimu tulipata wakati mgumu lakini nashukuru uwapo wa Benzema. Anafanya kazi yake vema,” alisema Perez.

Benzema alikuwa chachu ya kikosi hicho katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Girona ambao uliwawezesha Madrid kutinga nusu fainali ya Copa Del Rey.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles