23.2 C
Dar es Salaam
Saturday, October 12, 2024

Contact us: [email protected]

Scholes: Berbatov alitabiri Martial kuwika

MANCHESTER, England

MKONGWE wa Manchester United, Paul Scholes, amefichua kuwa Dimitar Berbatov, aliwahi kumwambia kuwa Anthony Martial atakuwa habari nyingine na ndicho kinachotokea.

Martial raia wa Ufaransa, ameongeza mkataba wa miaka mitano kuendelea kucheza Man United baada ya kuonyesha kiwango cha juu chini ya kocha wa muda, Ole Gunnar Solskjær.

Mkataba wake mpya utakaombakiza klabuni hapo hadi mwaka 2024, unamfanya sasa awe na uhakika wa kukunja kitita cha pauni 200,000 kwa wiki.

Akizungumza na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Scholes, anasema miaka mingi iliyopita aliambiwa na Berbatov kuwa Martial ana kipaji kikubwa, hivyo si ajabu akawa gumzo katika siku za usoni.

“Nakumbuka niliwahi kuzungumza na Berbatov, akaniambia Martial atakuwa mchezaji wa daraja la juu hapo baadaye.

“Aina ya uchezaji wake, namna anavyokokota mpira, alikuwa vizuri sana,” alisema Scholes akikumbushia kipindi ambacho Martial alikuwa Monaco.

Martial alitua Old Trafford mwaka 2015 na kocha aliyemsajili ni Louis van Gaal, ambapo katika mechi yake ya kwanza iliyokuwa dhidi ya Liverpool alifunga mabao mawili.

Hata hivyo, mchezaji huyo alijikuta akipoteza nafasi katika kikosi cha kwanza cha Mashetani Wekundu chini ya kocha Jose Mourinho, hivyo kuzua shaka kuwa angeondoka zake.

Tangu alipoanza kutinga ‘uzi’ wa Man United, Martial, ameshapachika mabao 46 katika mechi 161 alizoshuka dimbani.

Kocha Solskjaer anaamini Martial atafuata nyayo za mshindi mara tano wa tuzo ya Ballon d’Or, Cristiano Ronaldo, ambaye alipita Man United kabla ya mafanikio hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles