Papa Sapere kuja na kitu ‘Slowly’

0
451

Na CHRISTOPHER MSEKENA

BAADA ya kufanya vizuri na wimbo, Why Me, msanii wa kizazi kipya anayeishi Rockford, Illinois nchini Marekani, Love Evariste a.k.a Papa Sapere, amewaomba mashabiki kukaa tayari kwa ujio wa ngoma mpya, Slowly.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Papa Sapere alisema wimbo, Slowly utatoka rasmi Jumamosi hii katika mitandao yote ya kusikiliza na kuuza muziki hivyo mashabiki wajiandae kupata burudani.

“Kikubwa mashabiki wanaweza kutembelea chaneli yangu ya YouTube na ku-subscribe ili nikiachia video ya Slowly waweze kuipata, mimi ni msanii mpya ila ninaamini nina kipaji kikubwa cha kukonga nyoyo za mashabiki zangu kupitia ‘project’ hii,” alisema Sapere.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here