29.9 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Kings Msafiri atamba na ‘Yesu ni Wangu’

GEORGIA, MAREKANI

KUTOKA Georgia, Marekani mwimbaji wa Injili anayefanya vizuri pande hizo Kings Msafiri, ametamba kuwa wimbo wake, Yesu ni Wangu umemfungulia milango mingi ikiwa ni pamoja na kupata mashabiki wapya.

Kings ameliambia MTANZANIA kuwa hapo awali alikuwa hafikirii kama muziki wake unaweza kufika Afrika hasa Afrika Mashariki ili baada ya kutoa wimbo huo, Septemba, mwaka huu amekuwa akipokea shuhuda nyingi kutoka sehemu mbalimbali duniani.

“Wimbo Yesu ni Wangu umenifungulia milango mipya, namshukuru Mungu kwa kuendelea kukuza huduma yangu ya uimbaji naamini nitaendelea kufanya vizuri sio tu hapa Marekani bali hata huko Afrika,” alisema Msafiri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles