33.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

J Bwai aiweka wazi ‘Busy Body’

NA CHRISTOPHER MSEKENA

MWANAMUZIKI nyota kutoka Canada, Michael Baiye ‘J Bwai, amewaomba mashabiki wa muziki huo kuipokea audio ya wimbo, Busy Body aliouachia jana katika mitandao yote ya kusikiliza na kuuza muziki.

Akizungumza na MTANZANIA, Bwai alisema anamshukuru Mungu mapokezi yamekuwa mazuri ingawa bado anawaomba mashabiki kutoka Tanzania na Afrika Mashariki kuendelea kumpa sapoti.

“Tayari nimeachia Busy Boy kwenye mitandao yote ya kusikiliza na kuuza muziki hasa katika chaneli yangu ya YouTube. Naamini nina mashabiki wengi Afrika kwahiyo naomba wanipe sapoti nizidi kufanya vizuri,” alisema J Bwai mwenye asili ya Cameroon.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles