Papa Francis aanguka Kanisani

Papa Francis akijitahidi kunyanyuka baada ya kuanguka.
Papa Francis akijitahidi kunyanyuka baada ya kuanguka.
Papa Francis akijitahidi kunyanyuka baada ya kuanguka.

CZESTOSHOWA: Poland

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis (79) jana alianguka wakati wa ibada,   kwenye madhabahu ya Jasna Gora, mjini Czestoshowa, Poland.

Tukio hilo lilitokea  baada ya Papa Francis kujiikwaa akiwa madhabahuni hali iliyowalazimu mapadre waliokuwa karibu naye kumsaidia kuinuka.

Taarifa zinasema Papa alianguka chini karibu na ngazi za madhabahuni na aliinuliwa na mapadri waliokuwa kwenye misa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa za utabibu, Papa Francis amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa sciatica unaosababishwa na  maumivu chini ya mgongo.

Papa Francis, ambaye ni mzaliwa wa  Argentina alionekana akitembea huku akitafakari  hali iliyomfanya asigundue kuwa kulikuwa na ngazi mbele yake.

Baad ya kuinuka, Papa Francis, aliendelea na taratibu za ibada kama ilivyopangwa.

Alihubiri kwa muda mrefu kwenye ibada hiyo iliyohudhuriwa na maelfu ya waumini huku ikifuatiliwa pia na mamilioni ya waumini wa dhehebu hilo, kwa njia ya runinga.

Msemaji wa Vatican, Greg Burke, aliwaambia waandishi wa habari   kuwa kiongozi huyo yuko salama na hakuna maumivu yoyote aliyoyapata alipoanguka.

Papa Francis aliwahi kuteleza na hata kuanguka mara kadhaa   na kila mara huwa anainuka peke yake au kusaidiwa na mmoja wa wasaidizi wake,

Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki Duniani aliendesha   ibada katika kituo cha utawa ambayo ni nyumba maarufu ya watu kale  kwa Kanisa   Katoliki.

Katika ibada hiyo, ulinzi ulikuwa mkali kutokana muendelezo wa mashambulio ya ugaidi barani Ulaya.

Wanajeshi na polisi walionekana maeneo mbalimbali ya barabara katika ziara hiyo ya siku tano nchini Poland.

“Akili zetu zinarejea kwa vijana na binti wetu wenyewe, kama mashahidi waliosimama kwa nguvu zote wakiangazwa na  injili,   kama wale watu wa kawaida walioshuhudia upendo wa Bwana katika mateso makubwa,” alisema Papa Francis.

Papa Francis  aliwakumbuka watakatifu wawili wa  Poland, Mtakatifu Yohana wa pili na Faustina akisema: “Kupitia njia hizi za upendo wake, Bwana ametoa zawadi yenye thamani kubwa kwa Kanisa na kwa watu wote.”

Alitoa wito kwa raia wa Poland kuwa na umoja  kwa vile  taifa hilo  limegawanyika kuhusiana na masuala ya wakimbizi na wahamiaji, hasa wale ambao si Wakristo.

Papa aliongoza Ibada ya Misa ya kusherekea miaka 1050 ya imani ya  Kanisa   Katoliki katika kituo cha utawa Jasna Gora nchini humo.

Katika sherehe hizo inakumbukwa sanamu ya Black Madonna ambayo ilipelekwa nchini humo miaka ya 600 iliyopita.  Picha hiyo imechorwa kwenye mti na kuvishwa mkufu wa kahawia.

Sanamu ya Black Madonna ambayo  imekuwa ikiheshimiwa tangu mwaka 1711, inafahamika kuwa ilipofikishwa  kwenye cha utawa cha Jasna Gora ilizuia vifo kusini mwa nchi hiyo.

Picha hiyo iliyochora na mwanafunzi wa Yesu Kristu, mtume Luka, inasifiwa kwa miujiza.

Inasemekana makovu mawili usoni mwa Madonna yaliwazuia  majambazi walipotaka kuiba mwaka wa 1430,  wezi hao  walipokimbia  baada ya kuona damu inatoka kwenye picha hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here