23.7 C
Dar es Salaam
Sunday, October 1, 2023

Contact us: [email protected]

Mwigulu anasa Wachina 72 wakiishi kinyemela nchini

Mwigulu Nchemba
Mwigulu Nchemba

Na ALEX SAYI, GEITA

WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba, amefanya ziara ya kushtukiza katika Mgodi wa Dhahabu wa Nyamahuna mkoani  Geita na kukuta Wachina 72 kati ya 100 wakiishi na kufanya kazi bila vibali.

Akizungumza katika mgodi huo unaomilikiwa na Mtanzania, Andrew Obole, Mwigulu alisema alifika hapo kutokana na kuona taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya jamii.

Mwigulu alisema taarifa hizo zilimuonyesha Masanja Shokera akicharazwa bakora na raia wa mmoja wa China, Lee Swii, kwa madai ya kuiba mawe ya dhahabu Julai 6, mwaka huu.

“Nimefika kuthibitisha nilichokisikia kwamba kuna raia wa kigeni wanachapa watu hapa. Nimemuona mtuhumiwa wa udhalilishaji na kushangazwa na kukuta wafanyakazi wa China hapa wapatao 100 kwenye mgodi huo,” alisema.

Alisema taarifa alizonazo ambazo zipo uhamiaji zinaonyesha kuwa raia wa China waliopo mgodini hapo ni 28 ambao wana vibali halali vya kuishi nchini.

Waziri alisema kwa sababu hiyo, aliagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Geita kuwaweka chini ya ulinzi Wachina wengine 72, walinzi saba   na Kaimu Meneja Uzalishaji, Richard Joachim.

“Wakati hawa wakiwa chini ya ulinzi  naiagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Geita kuchunguza uhalali wa raia hao wa China kuishi nchini bila ya kuwa na vibali.

Vilevile  huyo anayeitwa Lee ambaye anatuhumiwa kumdhalilisha Mtanzania mwenzetu awekwe chini ya ulinzi na walinzi saba na kumpiga na kumjeruhi,”alisema.

Masanja Shokera ambaye anayedaiwa  kudhalilishwa,  , alisema  siku hiyo alivamiwa na walinzi wa mgodi huo  akituhumiwa kuiba mawe ya dhahabu.

Alisema walimpiga  na kumfunga mikono na miguu na kuendelea kumwadhibu hali iliyosababisha apoteze fahamu.

“Walionipiga wote nawatambua, ni hawa walinzi wa Kimasai wote walinishambulia na huyu Mchina alikuja pia kunipiga wakati nimefungwa kamba… alianza huyu mkuu wa ulinzi,  Sitta Dotto kuwaamrisha nikaguliwa kunipiga kichwani,” alisema.

Mkurugenzi wa mgodi huo, Andrew Obole    alisema anachotambua Wachina waliopo kwake ni 28 na kwamba hao wengine alikuwa hawatambui.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles