23.8 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

PANGA PANGUA KAMATI ZA BUNGE

Na Mwandishi Wetu-DAR ES SALAAM


SPIKA wa Bunge, Job Ndugai, amepangua kamati za Bunge, huku baadhi ya waliokuwa wenyeviti wa kamati za awali wakijikuta wakihamishwa.

Taarifa ya iliyotolewa jana na ofisi ya Spika wa Bunge, ilieleza mabadiliko hayo yamefanyika kwa mujibu wa Ibara ya 96 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 ambayo imelipa uhalali Bunge kuunda kamati za Bunge za namna mbalimbali kadiri itakavyoona inafaa kwa utekelezaji bora wa madaraka yake.

Aidha, ibara hiyo imeweka wazi kwamba Kanuni za Kudumu za Bunge zitafafanua muundo wa shughuli za kamati za Bunge.

Kwamba kutokana na msingi huo, Kanuni ya 118 ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016 imeweka kamati za kudumu za Bunge zenye muundo na majukumu mbalimbali kama yanavyofafanuliwa katika nyongeza ya nane.

“Uteuzi wa wabunge kwenye kamati mbalimbali umewekewa utaratibu katika Kanuni ya 116. Aidha, Kanuni ya116 (7) inaweka utaratibu kwamba ujumbe kwenye Kamati za Kudumu za Bunge utadumu mpaka mwisho wa Mkutano wa Kumi wa Bunge ambao ni nusu ya kwanza ya maisha ya Bunge.

“Mtakumbuka kwamba mnamo tarehe 21 Januari, 2016 kupitia waraka wangu Na.02/2016 nilifanya uteuzi wa ujumbe katika kamati mbalimbali za Bunge.

“Kamati hizo zimetekeleza majukumu yake mpaka Februari 9, 2018 ambapo ni mwisho wa Mkutano wa 10 wa Bunge ambao unakamilisha nusu ya Uhai wa Bunge Ia Kumi na Moja. Hivyo kwa mujibu wa Kanuni ya 116(7), kipindi hicho ndiyo ukomo wa ujumbe katika Kamati mlizokuwa mkifanya kazi,” alisema Spika Ndugai katika taarifa yake

Alisema kwa mamlaka aliyopewa na Kanuni ya 116(3) na kwa kuzingatia vigezo vilivyoanishwa katika Kanuni ya 116(5) amefanya uteuzi mpya wa ujumbe katika Kamati za Kudumu za Bunge.

Spika Ndugai alisema aajumbe wa kila kamati wanawajibika kuchagua Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti kwa mujibu wa Kanuni ya 116(10) kuwa viongozi wao.

Katika muundo huo Kamati ya Uongozi ya Bunge itakuwa chini ya uenyekiti wa Job Ndugai huku makamu wake akiwa ni Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson huku wajumbe wengine wakiwa ni kiongozi wa Shughuli za Serikali Bunge au Mwakilishi wake,  Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni au Mwakilishi wake, Mwanasheria Mkuu wa Serikali au Mwakilishi wake pamoja na wenyeviti wa kamati za Bunge.

Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge baadhi ya walioteuliwa ni Ramo Makani, Margareth Sitta, George M. Lubeleje, Dk. Suleiman Yussuf,  pamoja na aliyekiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulizni na Usalama, Balozi Adadi Rajab.

Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira baadhi ya wajumbe ni Ahmed Salum,  Hawa Mwaifunga David Mwambe huku Kamati ya Katiba na Sheria ni Upendo Peneza,  Asha Abdullah Juma,  George Simbachawene, Prof. Jumanne Abdallah Maghembe, Saed Kubenea na Tundu Lissu.

Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ni  Almasi Maige ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Bonna Kaluwa, Cosato Chumi, Fakharia Shomari Khamis na Mussa Zungu ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Huduma na Maendeleo ya Jamii.

Kamati ya Utawala na Serikali za Mitaa, Angelina Malembeka,  Anna Gidarya George Lubeleje na Hamad Salim Maalim huku Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii waliteuliwa ni  Bernadeta Mushashu, Grace Tendega, Peter Lijualikali, Hussein Bashe, Zitto Kabwe  na Peter Serukamba.

Kwa upande wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii ni Nape Moses Nnauye, Boniface Getere, Grace Kiwelu, Magdalena Sakaya huku Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji walioteuliwa ni Deo Sanga, Dk. Christine Ishengoma, Edwin Ngonyani na Justine Monko.

Kamati ya Miundombinu ni Abbas Ali Hassan Mwinyi, Ahmed Shabiby, Asha Mshimba Jecha, James Mbatia, Charles Kitwanga na Nuru Bafadhili huku Kamati ya Nishati na Madini Ally Kessy, Catherine Magige, Bahati Ali Abeid,  Dunstan Kitandula, Lameck Airo, Hamoud Jumaa na  Joseph Musukuma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles